Thursday, April 24, 2014
NAFASI YA KAMATI ZA DAAWA MASHULENI KATIKA MALEZI YA WANAFUNZI
(Mada iliyowasilishwa katika Semina iliyoandaliwa na mashababu wa Hizb kujadili nafasi ya Kamati za Daawa. Tarehe 19/04/2014. Haile-Salassie- Zanzibar)
Kumekuwa na ongezeko kubwa la matukio ya kushtusha na kutisha kutokana na kuporomoka maadili katika taasisi nyingi za kielimu ikiwemo mashuleni katika nchi za kimagharibi. Nchi hizi hasa Marekani na nchi za Magharibi kwa ujumla ambazo tunaziona eti ndio za kuigwa na kigezo chetu ‘role model’. Nchi hizi zimefeli kabisa katika kuwalea wanafunzi wao kwa maadili bora na hivyo mashule yao kubadilika kuwa uwanja wa mauaji. Ni hivi majuzi tu! tumeshuhudia janga la mwanafunzi aliyewachoma kisu na kuwajeruhi wanafunzi wenzake kumi na tisa katika skuli ya Sekondari ya Pennsylvania nchini Marekani (http://timesofindia.indiatimes.com/world/us/Student-goes-on-a-stabbing-spree-in-US-school-attacks-19-fellow-pupils-and-a-security-guard/articleshow/33510472.cms)
Aidha, bado tunazo kumbukumbu za kijana Adam Lanza wa huko huko Marekani aliyegonga vichwa vya habari katika mwaka 2012 kwa kuwaua wanafunzi ishirini na walimu sita katika shule ya Sandy Hook ndani ya jimbo La Connecticut. (en.wikipedia.org/wiki/Sandy_Hook_Elementary_School_shooting )
Hayo ni katika nchi zinazoitwa vinara wa ustaarabu. Hata hivyo nchini kwetu na ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla nako kumejaa matukio ya utovu wa nidhamu na kuporomoka kwa maadili miongoni mwa wanafunzi kama vile: uzinifu, liwati, ulevi, uvutaji bangi, utumiaji wa madawa ya kulevya, matendo ya utumiaji wa nguvu (violence),unyanyasaji wa wanafunzi kwa wanafunzi (bulliying), wanafunzi kujinyongan nk. Katika kuongezeka mimba za mashuleni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu aliwahi kusema kuwa Wizara inapambana na changamoto kubwa ya mimba mashuleni. Serekali imebaini jumla ya wanafunzi 8000 hupachikwa mimba kila mwaka (Habari leo 30 Nov 2013) Na kwa upande wa Zanzibar ndani ya miaka mitano kuanzia 2008-2012 wasichana 659 waliacha masomo katika mikoa mitano ya Zanzibar ambapo 277 ni kutokana na ujauzito (Waziri wa Nchi Afisi ya Raisi Zanzibar Dr. Mwiny Haji Makame) Hii ni ithibati tosha kwamba nidhamu ya kielimu ndani ya mfumo wa Ubepari imeshindwa kutoa wanafunzi wenye maadili bora ambao ndio wazazi wa baadae.
Ni katika hali kama hii ya kuporomoka kwa maadili mashuleni na taasisi za elimu kwa ujumla ndipo ambapo kunahitajika kuwepo Kamati za daawa ambazo angalau kwa uchache zitaweza kutoa nasaha na kuwakumbusha wanafunzi wajibu wao na malengo yao ya kuwepo mashuleni.
Kamati za daawa zinaweza kutoa mchango mkubwa katika kulea, kuongoza, kunasihi na kuwaidhi wanafunzi na kuweza kupata ufanisi lau kama zitapata mikakati bora, wanaharakati weledi na muongozaji hodari atakaezisimamia na kuzielekeza vizuri. Kamati hizi zinaweza kuwa chachu muhimu ya kuwahamashisha wanafunzi kusoma kwa bidii na mwishowe kufaulu mitihani yao. Hili linawezekana kwa kamati hizi kuandaa program/‘activities’ mbalimbali zitakazowaelemisha na kuwachangamsha wanafunzi. Baadhi ya mambo hayo ni kuandaa mihadhara/mawaidha na kuwaalika wahadhiri mbali mbali, kuandaa midahalo ‘debates’ kati ya wanafunzi au baina ya shule moja na nyengine, kuanzisha maktaba ‘libraries’ ambapo wanafunzi watafaidika kwa kusoma vitabu, majarida na machapisho tofauti.
Sisi ndugu zenu wa harakati ya Kiislamu ya Hizb ut-Tahrir tumejitokeza wazi kunyoosha mikono yetu kuchukua nafasi adhimu ya kuzielekeza, kuziongoza na kuzisaidia kamati za daawa mashuleni na vyuoni pale panapostahiki kupitia kuandaa vikao/semina, mihadhara, kuchawanya vipeperushi na matoleo mbali mbali yanayolenga kuwafahamisha wanafunzi majukumu na nafasi yao katika kuulinda na kuutetea Uislamu wakiwa katika taasisi za elimu au nje ya taasisi hizo. Aidha Sisi kwa kupitia kamati hizi tutasaidia kutoa ufahamu sahihi wa Uislamu kama mfumo kamili wa maisha na kukosoa ufahamu mbovu na wa kimakosa ulioenea katika jamii yetu. Basi ni wajibu kamati nazo kuchukuwa fursa hii kwa kufanya kazi nasi kwa maslahi ya Uislamu
NAFASI YA KAMATI ZA DAAWA MASHULENI KATIKA MALEZI YA WANAFUNZI (Mada iliyowasilishwa katika Semina iliyoandaliwa na mashababu wa Hizb kujadili nafasi ya Kamati za Daawa. Tarehe 19/04/2014. Haile-Salassie- Zanzibar) Kumekuwa na ongezeko kubwa la matukio ya kushtusha na kutisha kutokana na kuporomoka maadili katika taasisi nyingi za kielimu ikiwemo mashuleni katika nchi za kimagharibi. Nchi hizi hasa Marekani na nchi za Magharibi kwa ujumla ambazo tunaziona eti ndio za kuigwa na kigezo chetu ‘role model’. Nchi hizi zimefeli kabisa katika kuwalea wanafunzi wao kwa maadili bora na hivyo mashule yao kubadilika kuwa uwanja wa mauaji. Ni hivi majuzi tu! tumeshuhudia janga la mwanafunzi aliyewachoma kisu na kuwajeruhi wanafunzi wenzake kumi na tisa katika skuli ya Sekondari ya Pennsylvania nchini Marekani (http://timesofindia.indiatimes.com/world/us/Student-goes-on-a-stabbing-spree-in-US-school-attacks-19-fellow-pupils-and-a-security-guard/articleshow/33510472.cms) Aidha, bado tunazo kumbukumbu za kijana Adam Lanza wa huko huko Marekani aliyegonga vichwa vya habari katika mwaka 2012 kwa kuwaua wanafunzi ishirini na walimu sita katika shule ya Sandy Hook ndani ya jimbo La Connecticut. (en.wikipedia.org/wiki/Sandy_Hook_Elementary_School_shooting ) Hayo ni katika nchi zinazoitwa vinara wa ustaarabu. Hata hivyo nchini kwetu na ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla nako kumejaa matukio ya utovu wa nidhamu na kuporomoka kwa maadili miongoni mwa wanafunzi kama vile: uzinifu, liwati, ulevi, uvutaji bangi, utumiaji wa madawa ya kulevya, matendo ya utumiaji wa nguvu (violence),unyanyasaji wa wanafunzi kwa wanafunzi (bulliying), wanafunzi kujinyongan nk. Katika kuongezeka mimba za mashuleni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu aliwahi kusema kuwa Wizara inapambana na changamoto kubwa ya mimba mashuleni. Serekali imebaini jumla ya wanafunzi 8000 hupachikwa mimba kila mwaka (Habari leo 30 Nov 2013) Na kwa upande wa Zanzibar ndani ya miaka mitano kuanzia 2008-2012 wasichana 659 waliacha masomo katika mikoa mitano ya Zanzibar ambapo 277 ni kutokana na ujauzito (Waziri wa Nchi Afisi ya Raisi Zanzibar Dr. Mwiny Haji Makame) Hii ni ithibati tosha kwamba nidhamu ya kielimu ndani ya mfumo wa Ubepari imeshindwa kutoa wanafunzi wenye maadili bora ambao ndio wazazi wa baadae. Ni katika hali kama hii ya kuporomoka kwa maadili mashuleni na taasisi za elimu kwa ujumla ndipo ambapo kunahitajika kuwepo Kamati za daawa ambazo angalau kwa uchache zitaweza kutoa nasaha na kuwakumbusha wanafunzi wajibu wao na malengo yao ya kuwepo mashuleni. Kamati za daawa zinaweza kutoa mchango mkubwa katika kulea, kuongoza, kunasihi na kuwaidhi wanafunzi na kuweza kupata ufanisi lau kama zitapata mikakati bora, wanaharakati weledi na muongozaji hodari atakaezisimamia na kuzielekeza vizuri. Kamati hizi zinaweza kuwa chachu muhimu ya kuwahamashisha wanafunzi kusoma kwa bidii na mwishowe kufaulu mitihani yao. Hili linawezekana kwa kamati hizi kuandaa program/‘activities’ mbalimbali zitakazowaelemisha na kuwachangamsha wanafunzi. Baadhi ya mambo hayo ni kuandaa mihadhara/mawaidha na kuwaalika wahadhiri mbali mbali, kuandaa midahalo ‘debates’ kati ya wanafunzi au baina ya shule moja na nyengine, kuanzisha maktaba ‘libraries’ ambapo wanafunzi watafaidika kwa kusoma vitabu, majarida na machapisho tofauti. Sisi ndugu zenu wa harakati ya Kiislamu ya Hizb ut-Tahrir tumejitokeza wazi kunyoosha mikono yetu kuchukua nafasi adhimu ya kuzielekeza, kuziongoza na kuzisaidia kamati za daawa mashuleni na vyuoni pale panapostahiki kupitia kuandaa vikao/semina, mihadhara, kuchawanya vipeperushi na matoleo mbali mbali yanayolenga kuwafahamisha wanafunzi majukumu na nafasi yao katika kuulinda na kuutetea Uislamu wakiwa katika taasisi za elimu au nje ya taasisi hizo. Aidha Sisi kwa kupitia kamati hizi tutasaidia kutoa ufahamu sahihi wa Uislamu kama mfumo kamili wa maisha na kukosoa ufahamu mbovu na wa kimakosa ulioenea katika jamii yetu. Basi ni wajibu kamati nazo kuchukuwa fursa hii kwa kufanya kazi nasi kwa maslahi ya Uislamu.
Subscribe to:
Comments (Atom)