KWA HABARI NA UCHAMBUZI WA UHAKIKA,KITAIFA NA KIMATAIFA,USIKOSE KUTEMBELEA BLOG HII.

MAKALA


"MWAKA MPYA" MBINU YA WANADEMOKRASIA KUSAHAULISHA MALENGO YA UMRI .

Hamza S. Sheshe
Mwaka 325 AD Kanisa Katoliki lilifanya mkutano mkuu wa kwanza huko Nicea. Mkutano huu uliitishwa na Mfalme Constantine (mpagani) ili kutuliza hali ya machafuko iliyosababishwa na wakristo waliokuwa wakipinga falsafa ya uungu iliyoasisiwa mwanzoni na Justin Martx, (Yusto). Huu pia ndio mkutano ulioanzisha misingi ya aqeeda ya ukristo wa leo iliyohusisha ‘utatu mtakatifu’, ‘dhambi ya asili’ na kufufuka kwa Yesu. Aidha, ndilo Baraza hili la Nicea lililoweka msingi wa Kalenda iliyokuja kuitwa Kalenda ya Gregorian kwa kulazimisha Wakiristo wote washerehekee Pasaka siku moja. Misimamo ya Baraza la Nicea ilipingwa vikali na baadhi ya Wakiristo ikabidi kanisa kuomba msaada kwa serikali (ya kipagani) isaidie kurejesha amani na utulivu. Katika upinzani huu waliteswa maelfu kama si malaki ya Wakiristo na wengi kuuwawa. Mabaki ya vifaa vya kutesea bado vinapatikana katika jumba la makumbusho huko Rhine, Ujerumani.
Kuanzishwa kwa kalenda ya Miladi ya Papa Gregory XIII lilikuwa ni jaribio la kufanya marekebisho kalenda ya Julian (iliyoanza mwaka 45BC) iliyokuwa ikitumiwa awali. Papa Gregory alisimamia mabadiliko haya, na rasmi katika tarehe 24 Februari 1582 akasaini waraka maalumu unaojulikana kwa jina la “Papal bull’ ili kuimakinisha kalenda hii :http://en.wikipedia.org/wiki/Gregorian_calendar.
Wakatoliki waliikubali kalenda hii kwa kuwa waliamini kwamba dhamira ya Mkutano wa Baraza la Nicea ulioanzisha muundo mpya wa siku ya Pasaka ilikuwa pia kuanzisha kalenda mpya. Japo kwamba lengo la Mkutano lilikuwa ni kupata tarehe maalumu ya kusherehekea Pasaka kwa Wakiristo wote kwa pamoja. Kabla ya hapo Pasaka ilikuwa ikisherehekewa mwezi wa habib ( unavyojulikana katika Bibilia )uliokuwa ukiisabiwa kwa kalenda ya mwezi. Lakini kwa kuwa muandamo wa mwezi hubadilika badilika ndipo Kanisa Katoliki likafanya mabadiliko makubwa ndani ya mwaka 325. Mabadiliko ambayo yalitoa viashiria vya kubadilisha muundo mzima wa kalenda ambao baadae ulikuja kumakinishwa na Papa Greogry wa kumi na tatu.
Hata hivyo baadhi ya makanisa yasiyokubaliana na upapa wa Kikatoliki yalikataa kalenda hii.
Miongoni mwao ni Waporestanti na Kanisa la Orthodox. Mataifa mengine yalianza kuikubali kalenda hii kidogo kidogo, hata Khilafah Uthmaniya ilikubali kuitumia kalenda hii katika miaka ya 1890 wakati wa zama zake za uzorotefu, na kuibakisha kalenda ya Hijiria katika mambo ya kiroho na ibadat tu.Kama vile katika hesabu ya Ramadhani na Hijja. Hii ni baada ya kudorora kwa kiasi kikubwa kwa dola ya Kiislamu, kiasi cha baadhi ya Waislamu hususan wasomi walioathiriwa na fikra za kimagharibi kama vile mhasibu Morali Othman (Msomi wa Kiislamu aliyeathiriwa na umagharibi ) kupendekeza kutupilia mbali kalenda ya Hijiria kwa kudai ina usumbufu katika masuala ya hesabu za kifedha.
Suala la kalenda au kuhesabu siku ni jambo tu la kumuwezesha mwanaadamu kuweka kumbukumbu na malengo yake ya kiutendaji na haliingia katika masuala la kiutawala. Ndio maana, japo kuwa kalenda hii asili ni ya Kanisa katoliki , lakini inafuatwa/adopted na sehemu kubwa ya dunia kama si yote. Pamoja na ukweli kwamba si Ukatoliki unaotawala dunia leo. Na badala yake dunia inatawaliwa na mfumo wa kibepari/kidemokrasia. Kwa kuwa ukiristo kamwe sio mfumo wa kimaisha wenye sifa na uwezo wa kumtawalia mwanaadamu na wala hauna masuluhisho ya mambo ya kimaisha. Bali ni kijidini kinachojumuisha baadhi ya fikra za masuala ya kiroho tu.
Mfumo wa kibepari unazitumia sherehe za mwaka mpya kukuza na kuimarisha fikra zake za ‘uhuru’ kwa kiasi kikubwa na masoko ya kibiashara. Huhamasisha kusherehekea kwa namna tofauti kama kulewa, kuzini, kucheza miziki, kamari, kuleta vurugu nk. Aidha, wanaipotosha na kuidogosha hazina muhimu na yenye thamani ya umri wa mwanaadamu na kupongezana kwa kumaliza mwaka salama usalimini bila ya kuwaonesha watu dira na malengo ya umri huo.
Uislamu ni kinyume na Ubepari/Udemokrasia ambao huwafanya watu kutokujua lengo la kuwepo duniani. Wao huona kila kitu kinaishia hapahapa na hakuna hisabu ya matendo kwa Muumba. Na ndio maana itikadi ya Ubepari/Udemokrasia wao huona kwamba kama Muumba yupo basi baada ya kuumba na kumpa mtu akili amemuachia ajipangie mfumo wake anaoutaka maishani kwa faida na hasara ya mwanaadamu mwenyewe. Wala Muumba hana tena nafasi ya kumhisabu mtu huyu. Aidha, Uislamu kamwe haudandii sherehe zisizokuwa za Kiislamu kwa kuwa tayari una sherehe zake zilizowekwa na sheria.
Badala yake Uislamu umeweka wazi lengo la mwanaadamu katika maisha haya kwamba ni kumtumikia Muumba. Na kila dakika mtu ajihesabu kabla ya kuhesabiwa, sio kwa faida ya kimada bali katika kushikamana na maamrisho ya Muumba. Tathmini hiyo sio baada ya kumalizika mwaka. Bali ni kila dakika na kila siku. Yaani Muislamu ajihesabu kabla ya kuhesabiwa.
Waislamu lazima tukumbuke katika umri huu tuna jukumu la kuongoza ulimwengu:
وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا
“Na vivi hivyo tumekufanyeni umati bora ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe shahidi juu yenu” (TMQ 2:143)
Kwa bahati mbaya leo tunaishi chini ya mfumo wa kikafiri ulimwenguni kote. Licha ya kuwa ni faradhi kwetu kuishi chini ya dola ya Kiislamu ya Khilafah, na ni dhambi kubwa kuishi zaidi ya siku tatu nje ya dola hiyo. Leo ni mwaka wa 88, bado tupo chini ya utwaghuti wa kirasilimali na demokrasia ilhali baadhi bado hawajatanabahi wala kuamka. Kila siku inayopita inakatika sehemu ya umri wetu, tunasonga hatua mbele kuelekea mauti na kuhisabiwa na Allah Taala. Aidha, ni hatua moja nyuma ya muda wa kutekeleza majukumu tuliyofaradhishiwa na Allah SW. Basi jee wakati haujafika wa sisi Waislamu kuamka na kujizatiti katika majukumu yetu?




USANII NA UWONGO WA DHANA YA “UHURU WA HABARI NA MAONI

Na Kaema Juma
Wakati wa siku ya tarehe 3 Mei ndio Siku ya Uhuru kwa Vyombo vya Habari kimataifa, ni muhimu kufedhehi, kukashifu na kudhihirisha wazi wazi uwongo wa fikra na dhana ya uhuru wa habari na uhuru wa maoni.
Nidhamu ya kidemokrasia ina miito kadhaa kuhadaa waliwengu ikiwa ni mbinu ya kuumakinisha fikra zake. Miongoni mwa miito maarufu ni mwito wa uhuru wa maoni ambapo hunadiwa kwamba watu wako huria kutoa mawazo, fikra na miono yao. Na hivyo watu wengi wenye ufahamu duni wametumbukizwa kwenye dimbwi la mfumo batil wa kidemokrasia kutokana na mwito huu. Mabepari wameutumia mwito huu kama mbinu muhimu katika kufikia malengo yao.

Mataifa ya kimagharibi kupitia wanafikra wao kwa kudandia miito hii ya uhuru wa maoni na uhuru wa habari wamekuwa wanatoa kauli chafu za kuukashifu Uislamu, lengo msingi ni kuwafanya Waislamu wawe na shaka na Uislamu wao. Pia kuwafanya Waislamu waachane kuonyesha kwamba Uislamu ndio mfumo sahihi wa maisha ambao unatakiwa utabikishwe kisiasa kupitia serikali ya Kiislamu ya Khilafah. Unafiki huo wa magharibi hupelekea baadhi ya Waislamu kufungwa, wengine kutekwa na wengine kuuwawa kamwe. Wengi wao pindi wanapokamatwa hubambikiwa kesi za uwongo mfano kesi za ugaidi, uhaini na uchochezi. Wamagharibi katika kushindwa mpambano wa kifikra wa kutetea mfumo wao wamefikia hatua hata ya kuwafunga baadhi ya wanaharakati wa Kiislamu bila hata ya kuwafungulia mashitaka na kujisahaulisha dhana yao ya uhuru wa maoni. Baadhi ya wanaharakati maarufu amma waliofungwa, kupotezwa au kuawawa kwa kule kutoa tu maoni yao ni kama Naveed Butt, Abu hamza, Babar Ahmed, Abdullah Feisal, Aafia siddiqui, Aboud rogo, Samir Khan, nk. Wote wamejikuta kuwa ni wahanga wa usanii wa dhana ya uhuru wa maoni. Uhuru ambao umenyongwa kupitia sheria za ugaidi.

Wamagharibi kwa kudandia uhuru wa maoni na uhuru wa habari wamekuwa hawakemei wanaokashifu Uislamu au hata kuwafungulia mashitaka. Bali wamekuwa wanawahifadhi, kuwapa ulinzi na kuwaunga mkono wanaomkejeli Mwenyezi Mungu, Mtume Muhammad (SAAW) na dini ya Kiislamu. Hutoa kashfa zao na matusi yao kwa kupitia machapisho ya magazeti, vitabu, au hata filamu.

Sio muda mrefu tumeshuhudia wamagharibi wakitengeza filamu zilizojaa upotofu na udanganyifu dhidi ya Uislamu na Ummah kwa kuonyesha Uislamu kama dini ya ugaidi ambayo haina kheri isipokuwa mauaji tu kwa asiyekubaliana nayo. Aidha, katika miaka ya karibuni tumeshuhudia filamu ndani ya nchi za Magharibi kiasi cha kuonyeshwa kwenye kumbi za nchi hizo. Wakionyesha hadharani filamu chafu na na uchochezi dhidi ya Uislamu bila ya kujali kwamba kitendo hicho kinawaudhi Waislamu. Yote hayo huruhusu kwa kigezo cha uwongo cha uhuru wa maoni na uhuru wa habari. Tumeshuhudia Mtume(SAAW) alitukanwa kwa kuchorwa kikatuni nchini Denmark na aliyetenda uhalifu huo alilindwa na serikali ya Denmark kwa kigezo cha kutekeleza demokrasia ya uhuru wa maoni.

Pia tumeshuhudia Murtad Salman Rushdie alipotunga kitabu The Satanic Verses ambacho kinakashifu Quran tukufu kwamba ni kitabu cha majini na aya zake zinatokana na mashetani. Wamagharibi walimsifu na kumpa tuzo kadhaa kama mtunzi mahiri. Kwa bahati mbaya vibaraka katika mataifa ya Waislamu hakuna walichofanya zaidi ya kukaa vikao vya kisanii katika Umoja wa nchi za Kiislamu(OIC). Jumuiya ya kikoloni.

Uhuru wa kupata habari nao huminywa katika mfumo wa kibepari/ kidemokrasia. Kwaniwao huitoa taarifa fulani pale tu wanapoona kuna maslahi. Na wanaizuiya habari fulani ikiwa hali ni kinyume. Tumeshuhudia Waislamu tunavyonyimwa kupata taarifa sahihi juu ya qadhia mbalimbali za waislamu wenzetu, kwa kupewa habari za upotofu. Maeneo mengi ambayo Waislamu wanadhulumiwa kwa kuvamiwa ardhi zao na makafiri huwa hawapati taarifa sahihi juu ya yanayoendelea. Vyombo vya habari vimekuwa vinawaita Waislamu wanaopigana kutetea biladi zao, heshima zao, watu wao na dini yao kwa majina ya siasa kali au magaidi. Waislamu wengine wamekuwa wanakamatwa na kufungwa jela kutokana na kuwa na cds zinazoonyesha matukio ya Waislamu wanaotetea miji yao, kwa kisingizio ati ni vifaa vya kuendelezea ugaidi ilhalli mafunzo ya kijeshi yanapatikana katika filamu mbalimbali ambazo huuzwa kihalali na zinazopatikanwa madukani. Aidha, Waislamu wengine kama dada yetu Samina Malik ambaye alikamatwa na cds za matukio ya Afghanistan na ramani ya miji ya Uingereza amefungwa jela ati kwa kosa la kukutwa na vifaa vya kusaidia ugaidi.

Huo ndio uwongo shahir dhahir wa dhana za “uhuru wa habari” na uhuru wa maoni. Na uwongo huo ni jambo la kutarajiwa kwa kuwa mfumo uliotowa fikra hizo za uhuru ni mfumo batil na wa uwongo.

Kwa hivyo njia ya kujiondowa katika fiklra hizo za uwongo ni kufanya kazi kuondosha mfumo wa kidemokrasia katika uso wa dunia na kuweka mfumo mbadala wa Uislamu chini ya kivuli chake cha dola ya Kiislamu ya Khilafah
 





UPOFU WA SIKU YA MADENI DUNIANI
Na Hamza Sheshe
Imekuwa kawaida kwa ulimwengu huu unaotawaliwa na mfumo wa kibepari/ kidemokrasia kuwawekea watu sherehe na kumbukumbu nyingi za kuadhimisha kwa sura ya majonzi, kujifariji na kujipumbaza. Haya huoneshwa ni katika juhudi za kuwanasua raia na ugumu wa maisha ilhali kumbe ni kuzidi kuulaza Ummah usione madhila ya mfumo huu batil.
Ni katika hali kama hiyo kila ifikapo tarehe 16 Mei ya kila mwaka huwa ni siku ya Madeni Duniani. Taasisi, mashirika na makampuni mbalimbali hujumuika kwa namna mbalimbali ili kuona namna gani madeni yanapungua. Cha kustaajabisha ! wote hawajadili kwa nini madeni yanaongezeka. Wamefanywa kuamini kuwa madeni ni sehemu ya maisha yao, yaani hayaepukiki.
Katika kutafuta suluhisho la madeni wamefikia mwisho wa upeo wao kwani madeni huongezeka kila siku, sio tu kwa watu binafsi bali kwa mashirika, na kubwa zaidi yanaongezeka kwa mataifa ulimwenguni. Tofauti ni asilimia tu ya madeni hayo.
Deni ni kitu chochote ambacho mtu mmoja au kikundi hupaswa kulipwa kutoka kwa mwengine baada ya kukichukua kwa makubaliano maalum. Anayekopa huwa ana tatizo ambalo hubidi aombe msaada kwa mkopeshaji ili kutatua tatizo lake kwa makubaliano maalum ya kurejesha baadae. Kimaumbile jamii haiwezi kuwa na watu wenye hali sawa za kiuchumi, afya na mengine na huhitajiana ili kukamilisha palipopungua. Kwa hiyo, lazima kuwe na makundi mawili (mkopaji na mkopeshaji) pia iwepo shida(uwezo duni wa kutatua changamoto).
Mfumo wa kibepari ambao umejengeka juu ya dhana ya kibinafsi zaidi umeongeza pengo kubwa baina ya mwenye nacho na asiyenacho(tajiri na masikini). Lengo ni kumfanya masikini kuwa tegemezi kwa tajiri.Hivyo maskini hukopa kwa masharti yatayomfanya daima kunyenyekea kwa tajiri. Madeni ni fimbo ya kumchapia mdaiwa. Hata mikakati yao ya kupunguza umasikini ni kuwachezea shere watu kwani kiuhalisia inaongeza ukali wa maisha. Na nchi maskini hupewa inayoitwa mikopo ya kujinasua kutoka katika umasikini ila kiuhalisia ni ‘danganyatoto’ kwani mikopo hiyo ni njia tu ya kuzifanya nchi hizo zizidi kuwa tegemezi kwa mataifa makubwa. Mwandishi Dambisa Moyo katika kitabu chake cha ‘Dead Aid” anaonesha namna gani nchi masikini hususan za Bara la Afrika zinavyonyonywa na mataifa makubwa kupitia kinachoitwa ‘mikopo ya maendeleo’. Mikopo hii hurahisisha unyonywaji zaidi wa rasilimali za nchi zao kwa urahisi.
Kwa mfano, deni la taifa la Tanzania hadi Disemba mwaka 2013 ni shilingi trilioni 27 (deni la nje ni trilioni 20.23 na la ndani ni trilioni 6.81). Sababu iliyoelezwa na Waziri wa Fedha Bi Sada Mkuya ni kutokana na riba kubwa tena ya kulimbikiza inayoendelea kuzaa (compound interest). Na ufumbuzi wake wanaona ni kukopa kwa nchi nyengine zenye riba ndogo ili kuzuiya deni lisipae na sio kuliondoa). Cha kuchekesha katika ulimwengu huu wa takwimu ulituonesha kwamba uchumi wa Tanzania ulipanda kwa asilimia 6.5 ndani ya mwaka huo 2013. Ikiwa ni pungufu ukilinganisha na mwaka 2012 ambapo uchumi ulipanda kwa asilimia 7.2. Vipi uchumi ukue, na deni liongezeke. Bila ya shaka hiki ni kiinimacho.
Wengine hutoa hoja kuwa madeni yanaongezeka kwa sababu ya utawala uliopo kama baadhi ya wanademokrasia na wachumi wao wanavyodai. Hali ya kupanda kwa deni la taifa ni kitu cha asili tangu Tanganyika ‘kupata’ uhuru wa bendera. Na pia tangu iwe Tanzania deni limekuwa likiongezeka tofauti ni kasi yake. Mfano mwaka 2005 wakati utawala wa sasa unachukua nchi deni lilikuwa trilioni 10, na kufikia mwaka 2013 limefikia trilioni 27.
Na wala sio hoja kwamba ni chama kinachotawala kama ‘wapinzani’ wanavyodai. Hali inaonesha kufikia mwisho wa mwaka huu 2014 deni la Marekani (miongoni mwa matajiri wanademokrasia wakubwa wakopeshao Tanzania) linatarajiwa kufikia dola trillion 21 (wastani wa trioni 33,600 za kitanzania).
Bali kiini cha tatizo hili ni sera za mfumo mbovu wa kirasilimali/ kibepari katika uchumi. Kwa kuwa ulimwengu wote takriban umezama katika mfumo huu, basi tatizo la madeni haliepukiki kwa kuwa ni sehemu ya mfumo. Katika mfumo huu vyanzo vikuu vya mapato ya nchi ni kodi (kutoka kwa wafanyakazi wake, makampuni na mashirika), na mikopo kutoka ndani na nje ya nchi. Katika hili makusanyo ya riba pia ni msingi wa kipato. Hakuna zaidi ya vyanzo hivi kwani serikali haijishughulishi kufanya hata biashara ila kuwapa ‘wawekezaji’.
Hali hii ya riba ndio iliyopelekea nchi ya Marekani kukaribia kufilisika kama nchi ya Ugiriki. Na baadhi ya majimbo ya Marekani kama Detroit yalitangaza wazi kufilisika. Kwa watu binafsi ndio usiseme hadi wengine wanajinyonga. Wengi hupoteza makaazi yao baada ya kushindwa kulipa na wengine biashara zao hufa.
Kuongezeka kwa madeni, kama wamarekani wanavyolitazama humaanisha kushuka kwa maendeleo, kupungua kwa ajira, mishahara na usalama wa nchi, na ni kuelekea kufilisika/ kutoweka kabisa. Hali hii ndio hushuhudiwa duniani kote leo.
Tofauti na ubepari, Uislamu haufanyi umasikini wa mtu kuwa mtaji wa tajiri, bali ni ibada kwa tajiri kupunguza pengo la kipato baina yake na maskini, ikawekwa zaka ambayo ni lazima kwa tajiri kutoa. Uislamu ukaharamisha kwa nguvu zote uwepo wa riba. Na pale inapotokea kukopeshana ikiwa mdaiwa anashindwa kulipa huongezewa muda au kusamehewa, kitendo ambacho ni ibada yenye thawabu nyingi. Allah Taala Anasema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنْ الرِّبَا إِنْ كُنتُمْ مُؤْمِنِينَ (البقرة:).
“Enyi mlioamini, Muogopeni Mwenyezi Mungu na acheni kabisa yote yaliyo zidi (kwenu) katika riba (kuanzia leo na kuendelea), kama kweli nyie ni waumini (kikwelikweli)” (TMQ 2:278)
وَإِنْ كَانَ ذُو عُسْرَةٍ فَنَظِرَةٌ إِلَى مَيْسَرَةٍ وَأَنْ تَصَدَّقُوا خَيْرٌ لَكُمْ إِنْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ (البقرة:
“Na iwapo mdaiwa yupo katika hali ngumu (hana pesa za kulipa) muongezee muda hadi itakapo muwia rahisi kwake kukulipa, ila kama utamsamehe (deni hilo) kwa wema ni jambo jema sana kwenu iwapo mnatambua” ( TMQ 2:280)
Aidha, Uislamu unaharamisha kulimbikiza mali, kama pesa katika mabenki ili mzunguko wa fedha uwe mkubwa, pia umeondoa matumizi ya pesa ya karatasi ambayo thamani yake hubadilika badilika kwa mujibu wa maamuzi ya kikao. Badala yake Uislamu ukaweka pesa za madini ya dhahabu na fedha. Kwa bahati mbaya kuna baadhi ya Waislamu katika jamii wanapoteza Ummah kwa kuiga masuluhisho ya kibepari kama kuanzisha ati vyama vya kuweka na kukopa, au kuasisi zinazoitwa ati benki za Kiislamu nk.
Siku ya madeni duniani itaendelea kulaza Ummah bila ya faida yoyote. Watu watahangaika kubadilisha vyama lakini bila ya kubadili mfumo kiujumla (sio eti kieneo) hakutokuwa na mafanikio. Suluhisho la kudumu tuukatae ubepari tuikatae nidhamu yake ya kidemokrasia na kushirikii katika juhudi za kuirejesha tena dola ya Kiislamu ya Khilafah kwa kufanya ulinganizi wa kisiasa na kifikra usiotumia matumizi ya kinguvu kama alivyofanya Mtume Muhammad(SAAW).



OPERESHENI YA TANGA NA TARUMBETA LA UZUSHI.

Risala ya Wiki No. 245 Jumadal 1’ 1436 AH / Februari 2015
Masoud msellem.
Kufuatia operesheni ya Februari 14 iliyoendeshwa na Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la wananchi kukabiliana na uhalifu katika mapango ya Amboni, Tanga, kama kawaida na kitu cha kutarajiwa vyombo vingi vya habari vimepuliza kwa kishindo vuvuzela/tarumbeta la kuhusisha operesheni hiyo na magaidi, wakidokeza kuhusu kundi la Al-shabab.
Tunasema ni jambo la kusikitisha sana kwamba yanapotokea matendo ya uhalifu kama haya kwa haraka vyombo vya habari huyadandia na kuhitimisha kwamba ni Al-shabab au magaidi kwa makusudi hata kabla ya kukamilika uchunguzi ili kuulenga Uislamu na Waislamu.
Tunaweka wazi kwamba operesheni hii imedhihirisha zaidi kimbelembele endelevu cha baadhi ya vyombo vya habari namna vinavyochachamaa kubeba ajenda ya propaganda ya uadui dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Katika operesheni hii licha ya Jeshi la Polisi kukanusha kupitia Kamishna Paul Chagonja, kwamba waliokabiliana nao ni wahalifu na sio magaidi, na msimamo huo huo kusisitizwa tena na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Magalula Said Magalula, bado vyombo mbali mbali vya habari vilionekana kulazimisha kwa nguvu kubwa na kuimba wimbo wa magaidi na Al-Shabab.
Aidha, ilidhihirika baadhi ya vyombo kuhusisha operesheni hiyo na matukio ya uvamizi wa vituo vidogo vya polisi vya Mngeta, Kilombero, Morogoro na cha Bukombe, Mkoa wa Pwani. Matukio ambayo hata jeshi la Polisi halijawahi kamwe kuyahusisha na masuala ya ugaidi.
Tunauliza jee ikiwa jeshi la Polisi linaweka msimamo kwamba sio ugaidi. Kwa nini tena baadhi ya vyombo vishikilie na kulazimisha msimamo huo ikiwa havikubeba ajenda ya siri?
Lazima tuweke bayana kwamba vyombo hivyo vinabeba bango hilo la propaganda ili kuwatosa zaidi Waislamu licha ya madhara na misiba mikubwa inayotusibu kwa kaulimbiu ya uwongo ya ‘ugaidi’.
Tunapenda kukumbusha kwamba tangu Marekani ilipoilazimisha dunia hususan nchi changa zikiwemo nchi zetu za Afika Mashariki kupambana na Waislamu na Uislamu kwa ujanja wa tamko la ugaidi (vita dhidi ya Uislamu). Waislamu dunia kote ikiwemo katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki tunaishi kwa khofu, wasiwasi mkubwa na tumekuwa wahanga wa mauwaji, ,mateso na propaganda chafu.
Leo hata vile vyombo vya habari duni amma kwa kuburuzwa, kuajiriwa au kujipendekeza kwa madola makubwa hususan Marekani vinafuata sera ya kiuadui dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa kudandia na kulipinda kila tukio ili kuutosa Uislamu na Waislamu. Vyombo hivyo vikijisahau kwamba Waislamu ni miongoni mwa wateja wake wakubwa.
Aidha, tunakumbusha kwamba tabia hii ya baadhi ya vyombo vya habari kupayukapayuka kwa uadui dhidi ya Waislamu na Uislamu ni jambo la hatari ambalo huvuruga mahusiano mema baina ya watu, sio tu Tanzania bali dunia nzima.
Kwa kumalizia, ni wakati wa kutanabahi kwa baadhi ya vyombo vya habari, wanasisa na watendaji wao zikiwemo taasisi za ujasusi, ulinzi na usalama kwamba licha ya kubebeshwa na Marekani ajenda ya uadui na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Bado dola hiyo inazieka nchi zetu hizi, viongozi na watendaji wake kuwa ni watu wa daraja duni hata kuliko watumwa na wanazitazama nchi zetu, viongozi na raia wake kwa jicho la dharau isiyo na mfano. Hali hiyo hudhihirika katika miamala ya kila siku baina ya maafisa wa madola hayo makubwa hususan Marekani wanapokuwa na maafisa wa nchi zetu.Basi hili ni funzo la kutosha kwa nchi changa kama yetu kuacha uadui na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Uadui ambao kiudhati ni ajenda tu ya kubebeshwa na wengine.
www.hizb-eastafrica.com https://www.facebook.com/hizbeastafrica
02 Jamadal 1’ 1436 AH 21/02/2015 Miladi










 (Imetafsiriwa)
Taarifa kwa vyombo vya habari
Kusitisha mapigano maana yake ni kwenda sambamba na mbinu ya Marekani ya ufumbuzi wa kisisasa
Jana baadhi ya vyombo vya habari vilisambaza habari kuhusu mazungumzo ya kusitishwa mapigano ya mashariki ya Ghouta na baadae katika maeneo mengine.Achilia mbali kile kinachoitwa: ‘Mapatano au suluhu au kusitisha mapigano au...’ Kiuhalisia hayana maana yoyote zaidi ya utekelezaji wa mpango wa “Demistura” uliolenga kusitisha mapigano katika kanda fulani huku ikielekezwa nguvu katika maeneo mengine na kuendelea,ili kuandaa mazingira ya kukomesha mapinduzi na badala yake kuingiza mchakato wa kisiasa wa kuzalisha utawala wa kisekula wa kidemokrasia ambao utakuwa ni kibaraka wa Amerika.
Ni kana kwamba mapinduzi ya Shaam yalianzishwa tu dhidi ya mtawala katili hatimaye kufikia katika makubaliano ya pamoja na yeye juu ya meza moja ya mazungumzo ili kutekeleza mbinu ya utatuzi wa kisiasa ya Amerika.Na ni kana kwamba mapinduzi ya Shaam hayakuwa ya kujitolea kila kitu kwa vijana hodari kwa ajili ya kulinyanyua juu neno la Mwenyezimungu,na ni kana kwamba mapinduzi ya Shaam hayakuwa na mateso yoyote,ambayo watu wake hawakuwa si wenye kulazimika kuyakimbia makazi yao na heshima ya binti zao kuchezewa!!!
Marekani inafanya juhudi ya dhati kutaka kumfumba kila mtu,ikiwa ni pamoja na watu wa Shaam,kwa kutumia mbinu yake ya utatuzi wa kisiasa,utatuzi ambao ni makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa kwanza wa Geneva(Geneva 1) ambapo ulimwengu mzima ulidanganywa na kupumbazwa,bila hata kushauriana na wahusika kamili katika suala hili.Mbinu hii ya uatatuzi wa kisiasa ya Amerika inalenga kuzalisha serikali katika sura mpya chini ya misingi ya kisekula,kama walivyofanya hapo awali Tunisia,Misri na maeneo mengine.Hii ina maana kwamba tunarudishwa tena nyuma ya mraba mmoja kwa kurejea tena kuhukumiana kinyume na Uislamu chini ya uongo wa kidemokrasia,ambapo maamuzi ya mwanadamu yatakuwa yakitumika kutokana na mtazamo wa kimagharibi,ambao ni itikadi ya kutenganisha dini na maisha chini ya uongo wa kutambua haki ya mtu binafsi.Hii pia ina maana kwamba ukandamizaji,mateso na ugumu wa maisha utarudi kutawala ardhi yetu ambapo maneno ya Mwenyezi Mungu yatatumika juu yetu:-
﴿وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ
Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.{T’AHA :124}.
Je,iko wapi furaha chini ya kivuli cha mfumo wa kikafri,iko wapi haki baada ya kuondolewa haki ya Uislamu na sheria zake na nini tutasema kwa Mola wetu  pindi atakapotuuliza kuhusu damu ya mamia na maelfu ya mashahidi kwa kujtolea kwao kukubwa sana?
Yeyote atakayeifuatilia mbinu hii,mbinu ya utatuzi wa kisiasa ya Amerika,kutoka kwa wale waliokwisha jitumbukiza katika mstari wa kuwa zana wakatumika kwa ajili ya kufanikisha malengo ya kimagharibi,atagundua kuwa wamekosa kosa ambalo liko juu ya kiwango cha usaliti mkubwa,kwanza dhidi ya Uislamu na Waislamu,damu yao na dhabihu,Pili kwa wakati huu bahati mbaya wamechelewa.
Kwa hakika sisi Hizb ut-Tahrir katika wilayah ya Syria twawaonya,yeyote atakayejaribu kuingilia kati katika wa mapinduzi ambayo Ummah wa kiislamu umefungwa matumaini yake kwa ajili ya kufikia kwenye kile ambacho Allah(swt) amekiwajibisha juu yake,Khilafah iliyoongoka juu ya njia ya Utume.Sisi twawaonya,yeyote atakayejaribu kuwanyeyekea mabwana zake kwa gharama ya Neema za Mwenyezi Mungu(swt) na kwa gharama ya damu ya mashahidi na mateso ya watu wa Shaam.Sisi twamuonya mtu huyo kwamba ghadhabu ya Mwenyezi Mungu Al-Muntaqim Al-Jabaar kuwa itamkumba tu.Na tunasema kwamba makafiri wa magharibi watakutupa mkono baada ya kupata wanachokitaka kutoka kwako na baada ya hali itakapofikia kuwaneemesha,kama walivyowatupa kando wale wa kabla yenu,je yupo mwenye kuzingatia?
Allah(swt) amesema
﴿وَلَا تَكُونُوا كَالَّتِي نَقَضَتْ غَزْلَهَا مِن بَعْدِ قُوَّةٍ أَنكَاثًا
Wala msiwe kama mwanamke anaye uzongoa uzi wake baada ya kwisha usokota ukawa mgumu
{ An-Nahl: 92}.
﴿وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَا إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنتَقِمُونَ
Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye kumbushwa kwa Ishara za Mola wake Mlezi, kisha akazikataa? Hakika Sisi tutajilipiza kwa wakosefu
{ As-Sajdah: 22}
 

No comments: