Saturday, September 6, 2014
MWITO KWA MAKUNDI YA WANAMGAMBO NA MAKABILA/KOO ZINAZOPIGANA NDANI YA IRAQ NA SYRIA:KOMESHENI VITA BAINA YENU,AMERIKA INAPATILIZA KWA VITA HIVI KUTAKA KUINGILIA KIJESHI KATIKA NCHI YENU.
Kupamba moto kwa kasi kubwa kwa matukio ndani ya Iraq na Syria, hadi pia kusikika matamshi ya Obama tarehe 18/08/2014 na kusikika matamshi ya Waziri wake wa ulinzi Hegel pamoja na Jenerali Mkuu wa kijeshi Demsey, kama ilivyokuja kwenye mkutano wao na wanahabari tarehe 22/08/201 ukizungumzia kuhusu mkakati ulio na upeo mrefu wa kuingilia kijeshi katika nchi hizi... Mazungumzo hayo pia yaligusia hatua ya kuanzisha muungano wa kimataifa utakaounga mkono uvamizi huu wa kijeshi wa Amerika... Na yote haya ni baada ya kudhihirika maombi ya baadhi ya wakaazi wa maeneo hayo wakiwemo wanasiasa na wanajeshi wakiitaka Marekani iingilia kijeshi ati kuokoa hali hii! Na tayari Marekani imeanza kuingilia kupitia anga ndani ya Iraq. Tarehe 16/08/2014 Muungano wa Syria umeiomba kwa kusisitiza Amerika iingilie kijeshi Syria kama ilivyoingia Iraq. Muungano huo ukaiambia Amerika na kuilaumu Marekani kwa kuwa na sura mbili, kwanini inaingilia kijeshi Iraq na kuiacha Syria!
Waislamu na wakaazi wa eneo hili baada ya kuishi na kuona uadui na ushenzi wa Marekani na unyama wake kama ilivyoshuhudiwa Afghanistan na Iraq, mashambulizi ya ndege pasina rubani (drones) huko Pakistan na Yemen... leo hii ati ndio ati iombwe Marekani na itarajiwe kheri yake bali itakikane kwa haraka badala ya kukataliwa kuingilia kati kijeshi tena kwa ridhaa na khiyari za viongozi! Bila ya shaka hii ni shari mbaya zaidi ya shari ya kuingilia nchi za Kiislamu kwa nguvu na ujabari. Kama msemo unavyosemwa: Kushambuliwa na nyoka huku ukijitetea ni bora mara elfu kuliko kumleta nyoka kwa mkono wako nyumbani kwako kuuuwa wewe, watoto wako bali ni kila alioko ndani ya nyumba yako! Kwa hakika wanaotaka muangaza kutokana na moto wa Marekani (wanaotaka izza kupitia Marekani)macho yao yana vizibo, masikio yao yana uziwi na macho yao yana upofu!
Lakini ni kitu gani kinachosukuma muda na sehemu hii ikumbwe na matukio haya maovu? Na ni kitu gani kilichofanya Marekani aweze kufanya njama zote hizo na kutakuingilia kijeshi ? . Aidha ni lipi hasa lililofanya haya yawe ndio matakwa ya watu wa maeneo hayo wanaomtaka Marekani aingie tena tena wakitangaza hadharani pasina haya wala khofu? Mchunguzi makini atagunduwa kuwa Amerika inapatiliza mapigano baina ya harakati za kimapinduzi ndani ya Syria na Iraq. Baada ya harakati hizo kutoka kwa lengo la kuangusha matwaghuti kukabadilika wanaharakati wengi wakarudi nyuma ispokuwa wale waliorehemewa na Mwenyezi Mungu. Na hali ikabadilika kuwa mapigano baina yao kwa wao, wala sio mapigano baina yao dhidi ya makafiri wakoloni au baina yao na serikali ambayo awali walidhamiria kuibadilisha! Pamoja na yote hayo, pande zote mbili zinazopigana hasimami yoyote kujiuliza : Kwa nini yote haya yanatokea? Na ya wapi malengo yalikuwa yakidhamiriwa ambayo harakati hizi zimeundwa kwa ajili yake? Na vile vile hasimami yoyote miongoni mwa wanaharakati hao kujiuliza kwa mshangao: Kwa nini pande hizi zinazozana, ISIS na harakati nyengine? Kwa nini wanazozana juu ya maeneo ambayo tayari wameyakomboa kutoka kwa serikali badala ya kuzozana juu ya kuyakomboa maeneo mengine yanayodhibitiwa na serikali?!
Enyi Waislamu: Hakika sisi ndani ya Hizb ut-Tahrir msimamo wetu tunawalingania Waislamu walioko katika harakati ya ISIS, harakati zenye silaha na makabila wasitishe kupigana wao kwa wao, wafanye kazi ya kusuluhisha yaliomo baina yao. Wala wasimili kwa waliodhulumu nafsi zao ukaja ukawapata Moto... Twawalingania kwa mtazamo uliosheheni ghera/hamu ya kulinda maslahi ya Waislamu, kwa sababu ya maumivu, na huzuni ya kupasua mioyo yetu namna tunavyoona wapiganaji wa ISIS na harakati nyengine zote zikipiga takbira wakati wa kupigana kwao. Huku kila kundi likifanya bidii kulimaliza kundi jengine. Basi twawalingania wote hao huku tukigubikwa na machungu.... Basi tunatoa mwito huu kwenu tukiwa na matumaini na matarajio:-
Kwanza: Kwa Jumuiya ya ISIS, imche Mwenyezi Mungu kwa inayoyafanya, isitishe mara moja kuwauwa Waislamu, kwani damu ya Muislamu mbele ya Allah ni kubwa sana. ISIS itupilie mbali madai yake iliyoyatangaza ya kusimamisha Khilafah ya uwongo na kinyume cha sheria. Njia ya kusimamisha Khilafah yajulikana wazi wala sio kwamba haijulikani. Ameibainisha Mtume SAAW kwenye sira yake kwa uwazi mweupe, nayo ni kuomba nusra kwa wenye kumiliki nguvu katika nchi iliyo na sifa za serikali. Baadaye ifuate bai’a ya watu wa nchi ile hali ya kuridhia na kwa khiyari... Lakini hilo halikufanyika kwa ISIS. Haijachukua bai’a kwa mujibu wa ilivyoweka sharia. Na kila jambo linalofanywa kinyume na sheria basi hupelekea kwenye mizozo na fitina na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Matokeo yake mapigano yakaripuka baina yake na harakati nyengine na likatiwa fungamano baina yake na harakati nyengine ni fungamano la umwagaji damu . Ikawa kila mji unaoingia ISIS wakazi wake hutoroka badala ya kupata amani kutoka kwao. Basi tunailingania ISIS irudi nyuma na kutubu makosa hayo. Na kutubia makosa ni fadhila kubwa.
Pili: Kwa harakati nyengine zinazopigana kwa kuomba msaada wa Amerika, wamagharibi, vibaraka na wafuasi wao...Kutaka kwenu msaada kutoka kwa makafiri wakoloni ni makosa na pia huko ni kukosa uoni na mtazamo wa kina. Vipi Marekani au wamagharibi itawasaidia kuwaondoa vibaraka waliowaweka wao na sasa wanataka kuweleta vibaraka wapya wachukue mahala pao. Na kila mwenye akili timamu anafahamu hili. Ni kama mtu aliyotoka kutoka katika karai la mafuta na kuruka katika moto. Basi je hakuna mwenye kuzingatia miongoni mwenu?
Tatu: Enyi makabila... na waungwana katika watu... wenye hisia nzito za Kiislamu na mlio na heshima: msiunge mkono upande wowote katika makundi haya ya Kiislamu yanayopigana, kwani hata kama yametangaza dhamira ya vuguvugu lao ni kuondowa nidhamu za kitwaghuti na kutaka kuzibadilisha, lakini hawawapigi makafiri wakoloni bali wanapigana wao kwa wao. Na pia makundi haya hayaungani pamoja kukabiliana na nidhamu hizo. Wao wanachokifanya ni kukusanya tu vitimbi vyao katika kupigana wao kwa wao. Basi wanasihini kwa nguvu zenu zote na waunganisheni kwa uongofu ili mwelekeo wao uwe ni mmoja wa Kiislamu. Iwe inayokusudiwa ni Khilafah Rashidah ambayo chini ya kivuli chake watu watapata usalama na wala hawatojawa na khofu. Na watupilie mbali umajimbo, mgawanyo kwa misingi ya kimaeneo na kinchi.
Nne: Kwa wale ambao Allah Amewarehemu:
﴿إِلَّا مَنْ رَحِمَ رَبُّكَ﴾ “Ila wale ambao Mola wako Amewarehemu” (Hud: 119))
Waliotimiza ahadi waliyoahadiana na Mwenyezi Mungu na wakahadiana kumnusuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa lengo la kuisimamisha Khilafah Raashidah ...waliojitenga mbali kupigana dhidi ya harakati nyengine za Kiislamu, wakaendelea kufanya kazi ili kufikia lengo lao walilotokea kwa ajili yake.... Wakawa na istiqama juu ya haki ambayo nyinyi mumeshikana nayo wala msiathirike na wale wanaowaona nyinyi kuwa mko wachache, kuliko hizo harakati zinazomwaga damu ya Waislamu. Kwa hakika wachache wenye ikhlasi wana uzito mkubwa zaidi katika mizani ya Mwenyezi Mungu kuliko wengi walioko katika batili. Na mwisho mwema ni kwa wacha Mungu.
﴿وَنُرِيدُ أَنْ نَمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ﴾.
Na tukataka kuwafanyia ihsani wale waliodhoofishwa katika ardhi hiyo kuwafanya viongozi na kuwafanya warithi wa (neema hizo).
Enyi Waislamu: Hizb ut-Tahrir imeshapita kama miaka sitini ikiwa imesimama thabiti juu yaki inayoilingania. Ikijifunga na njia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu [SAAW] ya kuomba nusra ili kusimamisha hukmu /utawala wa Uislamu katika ardhi pasina na kupituka/kukengeuka kiasi hata cha unywele mmoja. Licha ya kusemwa sana na kuenezwa maneno mengi kuwa kuomba nusra ni njia ndefu na kuwa utumizi wa nguvu wa kulazimisha utawala kwa watu ndio njia fupi na karibu. Hawajafahamu wasemao maneno hayo kuwa suala sio kufikia tu kwenye utawala wowote, wala sio kwenda katika njia yoyote ile bali kadhia/suala hapa ni Khilafah kwa manhaj/ njia ya utume/unabii.
Na njia ni ile aliyoichora Mtume SAAW na akaiweka wazi na kuingaza vyema kwa wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Mwenye hekima... Na njia ya kinyume chake huenda ikafikisha kwenye utawala kwa muda fulani lakini utakuwa ni utawala mgonjwa usojimudu hauridhii Mwenyezi Mungu na Mtume wake wala Waumini....
Khilafah sio tamko tu lisilokuwa na madhumuni maalum bali Khilafah ya kweli ni iliyosalimika na kutulia, watu huhamia ndani yake kutafuta amani na usalama chini ya kivuli chake, wala sio ile inayoitwa Khilafah kwa jina tu ilhali watu wanaikimbia wakiwa na khofu na kuogopa kudhulumiwa. Khilifah ya kweli ni ile ambayo ndani yake watu watapata usalama wao na wa heshima zao mali na majumba yao. Wala hakumwagi damu na kuvunjwa heshima na kubomolewa majumba na kuporwa mali.... Ni Khilafah ambayo itaeneza kheri sio tu kwa biladi za Waislamu bali kwa wanadamu wote duniani. Na itabeba hadhara yake/ustaarabu kwa ulimwengu. Khilafah ambayo Waislamu na wasiokuwa Waislamu watakuwa na amani, na kila mwenye haki atapewa haki yake kwa udilifu na kwa kuridhika...
Kwa hakika Hizb ut-Tahrir ni kiongozi asiyedanganya watu wake, nayo inatokana nanyi na iko pamoja nanyi katika mwito huu. Inamlingania kila mwenye moyo wa ufahamu na akili ya utambuzi, na kwa kila mwenye masikio na kuwa makini: awekeze upeo wa juhudi hata kama nguvu yake ni kuzungumza nusu ya neno. Basi ajipinde kukomesha mapigano baina ya Waislamu kutoka ISIS dhidi ya harakati nyengine za kimapinduzi na pia zile za kikabila. Huenda wakati uliosalia ikasikizwa nasaha hiyo na mauaji yakakomeshwa, na wote wakawa safu moja kukabiliana na uvamizi wa Majeshi ya Muungano, mpango unaoratibiwa na kuongozwa na Amerika. Hatua hiyo ya kuacha mapigano baina yao itawafanya waweze kupambana na miungano hiyo na kuzuiya shari yao kabla hali haijawa mbaya zaidi... Mwito wetu huu kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu na kwa idhini yake ni mwito wa uaminifu na wa ikhlas. Tunamlingania kila mwenye moyo, msikivu makini/shahidi. Huenda akawa na dori/ nafasi kubwa yenye kuathiri katika kunusuru Uislamu na Waislamu na kuzuiya vitimbi vya makafiri wakoloni ...
Ama wale wasiosikia wala kuona, tayari Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu Asoshindwa ameshatujuza khabari zao
إِنَّ شَرَّ الدَّوَابِّ عِنْدَ اللَّهِ الصُّمُّ الْبُكْمُ الَّذِينَ لَا يَعْقِلُونَ
“Hakika vinyama viovu mbele ya Mwenyezi Mungu ni hawa wanaojipa uziwi (wakutosikia haki) wanaojipa ububu (hawasikii haki) ambao hawayatii akilini” (wanayoambiwa) [TMQ ANFAL: 22]
Hizb ut-Tahrir 28 Shawwal 1435 AH 24 Agosti 2014 Miladi
Subscribe to:
Comments (Atom)

