KWA HABARI NA UCHAMBUZI WA UHAKIKA,KITAIFA NA KIMATAIFA,USIKOSE KUTEMBELEA BLOG HII.

Thursday, October 23, 2014

Monday, October 13, 2014

NANI WA KUMUACHA HURU DK.AAFIA SIDDIQUI?

NANI WA KUMUACHA HURU DR.AAFIA SIDDIQUI?

Mwezi Machi 2009 Waandishi wa Habari wakike wawili wa Kimarekani, Euna Lee na Laura Ling walikamatwa na askari wa Jamhuri ya Korea ya Kaskazini wakati wakiripoti Habari mpakani mwa nchi hiyo na China kwa ajili ya kituo cha Televisheni “Current TV” chenye makao yake California . Hatimaye walihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 12 gerezani kwa kosa la "matendo ya kiuadui" na “kuingia kinyume cha sheria ndani ya Korea ya Kaskazini”.Baada ya kifungo chao serikali ya Amerika ilifanya kazi bila kuchoka ili kuwakomboa wanawake hao. Na ilipofika mwezi Agosti 2009 ikamtuma Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton ili kwenda kunena na rais wa Korea ya kaskazini Kim Jong Un. Mkutano huo ulizaa matunda na hatimaye wanawake hao wakaachiwa huru . Mnamo mwezi Machi 2003 alikamatwa mwanamke pia na kufungwa. Jina lake ni Aafia Siddiqui. Kama ilivyo kwa Waandishi wa Habari wa Kimarekani naye alikuwa ni mwanamke, ambaye alisoma na kufanya kazi hukohuko Amerika na watoto wake watatu walikuwa raia wa Marekani. Lakini tofauti yake na Waandishi wa Habari wa kimarekani yeye alitekwa miaka sita kabla ya waandishi hao pia yeye alikuwa Muislam ,ambaye hakuna kiongozi ambaye angeweza kushughulishwa masuala yake.
Hii ni historia yake kwa ufupi: Dr Aafia Siddiqui alizaliwa mjini Karachi, Pakistan, mwezi Machi 2, mwaka 1972. Yeye alikuwa mmoja wa watoto watatu wa Mohammad Siddiqui, daktari aliyepata mafunzo yake huko England, na mama yake Ismet ni mama wa nyumbani. Yeye ni mama wa watoto watatu ambao ni Ahmed(1996),Maryam(1998) na Suleman(2002).Aafia ni Hafidh-ul-Qur'an na ametunukiwa vyeti na shahada za elimu ya juu takriban mia moja kutoka vyuo mbalimbali duniani na ni mwanasayansi pekee wa kike duniani kufikia kupata Phd ya neuroscience katika chuo kikuu cha Havard-marekani . Aafia na watoto wake watatu walikamatwa na mawakala wa kiintelijensia wa Pakistani mnamo mwezi Machi 2003 na kukabidhiwa mbele ya Wamarekani nchini Afghanistan ambapo alifungwa katika gereza la Bagram na kubakwa mara kwa mara, kuteswa, na kunyanyaswa kwa muda mrefu huku mmoja wa watoto wake alikuwa ni mchanga akiwa na umri wa miezi kumi tu. Ripoti nchini Pakistani zilizoripotiwa katika vyombo vya habari kwa lugha ya Ki-urdu zinasema kuwa Aafia na watoto wake watatu waliweza kuonekana wakichukuliwa na mamlaka ya Pakistani na kuwekwa chini ya ulinzi .
Moazzam Begg, na mateka wengine kadhaa wa wamarekani wa zamani walitaarifu kwamba mfungwa huyo wa kike, "mfungwa namba 650",alifungiwa gereza la kambi ya kijeshi ya Bagram nchini Afghanistan.Yvonne Ridley wa Cageprisoners.com aliandika kuhusu "Mfungwa huyo namba 650" (Aafia) mateso yake na kurudia kubakwa mara kwa mara kwa zaidi ya miaka minne. "kilio cha mwanamke huyu mnyonge asiye na msaada kiliungwa mkono (pamoja na mateso ya aina hiyo) katika jela kiasi cha kusababisha wafungwa wote kuja juu na kuleta mgomo wa kukaa na njaa .Yvonne alimwita "mwanamke wa kijivu (gray lady)" kwa sababu alikuwa akigusa hisia za wengi , ambaye kilio chake na mayowe yake vitaendelea kuwagusa wote watakaopata kusikia sauti yake. Hii haitoweza kutokea kamwe kwa mwanamke wa kimagharibi.
Maofisa kutoka pande zote mbili,serikali ya Pakistani na Marekani walikanusha vikali madai yoyote ya utetezi kuhusu hatma ya adhabu ya kifungo cha Aafia,hadi pale ilipoanza kuleta hamasa kwa ummah na kwa baadhi ya vyombo vya habari kuanza kufuatilia habari yake.kisha likaletwa dai la kejeli na kipuuzi kuwa alihusika kwenye shambulizi la kigaidi la kuwashambulia askari wa kimarekani kwa bunduki.
Tarehe 4 Agost 2008,shirikisho la waendesha mashtaka nchini Marekani lilidai kuwa Aafia Siddiqui alipelekwa(extradited) Marekani kutoka Afghanistan ambapo wao wanadai kuwa walimuweka kizuizini tangu mwanzoni mwa julai 2008.Utawala wa Mrekani ulidai kuwa yeye(Aafia) alikamatwa na vikosi vya Afghanistan nje ya boma la mkuu wa mkoa wa Ghazni akiwa na makopo yaliyofungiwa kampaundi hatari za milipuko.Pia wanadai zaidi kwamba wakati wanajaribu kumuweka chini ya ulinzi aliwafyatulia risasi maofisa hao wa Marekani(hakuna hata mmoja aliyejeruhiwa) isipokuwa alijijeruhi yeye mwenyewe katika mchakato huo. Mnamo tarehe 7 Agosti,muhtasari katika taarifa za vyombo vya habari ziliweka wazi baadhi ya matibabu ambayo Aafia alikuwa anafanyiwa wakati yupo chini ya uangalizi wa Askari wa Kimarekani,ikiwemo na:
1.Figo yake moja iliondolewa
2.Meno yake yameondolewa
3.Pua yake imevunjwa na kushindwa kujirudi katika hali ya kawaida
4.Jeraha lake la risasi liliachwa wazi kwa muda mrefu bila kufunikwa mpaka ikapelekea nguo zake kutapakaa damu.
Ripoti ya Reuters ya tarehe 11 Agost 2008 ilisema kuwa Aafia alionekana akiwa mahakamani kizimbani huku wanasheria wake wakitaka vithibitisho vya kutosha juu ya matibabu yake.Mmoja wa wanasheria wake Aafia aliyejulikana kwa jina Elizabeth Fink alimueleza hakimu kuwa:

“(Aafia)amekuwepo hapa kwa muda wa wiki nzima bila ya kumuona daktari yeyote,pamoja ya kuwa wanatambua(utawala wa marekani) kuwa kapigwa risasi” Elizabeth Fink aliliambia jopo la mahakimu mjini New York kwamba inaonekana Aafia ana kila dalili ya kufanyiwa vitendo kinyume na utu wake kwa muda mrefu.Kwa mujibu wa nyaraka ilivyoelezwa katika mahakama hiyo na Fink,Aafia aliwaambia wafanya kazi wa gerezani kuwa anamhofia sana mwanawe kuwa huenda anateswa huku akiwa na njaa hivyo aliwaomba badala ya kumpa chakula yeye basi wakichukue chakula hicho kisha wamtumie mwanawe Afghanistan."

Wakili mwingine wa Aafia,Elaine Whitfield Sharp aliwahi kusikika akisema,

“Sisi tunajua kuwa yeye(Aafia) amekaa sana Bagram kwa muda mrefu,ni muda mrefu sana.Kulingana na mteja wangu yeye alikuwa huko kwa miaka akiwa chini ya ulinzi wa askari wa Marekani;matibabu yake yalikuwa duni mno”

Kwa miaka takriban 10 sasa mama huyu yupo kizuizini hali ya kuwa afya yake si nzuri huku akipata mateso kila kukicha,akibakwa na kufedheheshwa na kudhalilishwa chini ya Utawala wa kinyama wa Amerika na usaidizi wa hali na mali kutoka kwa vibaraka wake watiifu,utawala wa Afghanistan na Pakistan.Hatimye sasa amekataa kukutana na wakili wake,habari za kiafya zinasema kuwa kwa sasa anasumbuliwa na tatizo la uharibifu wa ubongo na kwamba sehemu ya utumbo wake imeharibika inaweza kuondolewa muda wowote.Wanasheria wake wanathibitisha hili kwa dalili wazi kabisa kwani amekuwa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu mno.
Kutokana na kukosekana kwa Khilafah yeye na waislam wote duniani ni wahanga wasio na ngao ya kujifichia na kama maneno ya mtume (s.a.w) aliposema kuwa sisi ni kama povu la sabuni na uchafu unaosukumwa mbali na mfereji wa maji. Kutoka kwa Thauban,Amesema mjumbe wa Allah kuwa: “Muda si mrefu watu watatafutana mmoja baada ya mwingine kupigana kama wafanyanyavyo watu wanapoitana kwenye chakula,” Mtu mmoja akauliza,je ni kwa sababu idadi yetu itakuwa ndogo wakati huo?,Mtume(s.a.w) akamjibu,”Hapana,mtakuwa wengi sana wakati huo:lakini ni sawa na mapovu ya sabuni na uchafu usukumwao na mfereji wa maji.Na Allah ataondoa woga kutoka katika nyoyo za maadui zenu na kuwatia Al-wahn katika nyoyo zenu ” Pia akaulizwa,ewe mjumbe wa Allah je ni nini hiyo Al-wahn,Mtume(s.a.w) akajibu “ni kuipenda sana dunia na kuogopa kufa”[Abu Dawud na Ahmad]
Ni wahn iliyoufanya utawala wa Pakistani kuwakamata wanawake wa kiislam na kuwakabidhi kwa Wamarekani,japokuwa mtume (s.a.w) ametuhusia kuwa: “Muislam ndugu yake muislam,hapaswi kumtendea ubaya(ujeuri) wala kumkabidhi kwa waonevu.Yeyote atakayemsaidia ndugu yake(muislam) Allah naye atamsaidia,Yeyote atakayemfariji ndugu yake(muislam) Allah naye atamfariji siku ya malipo.Na atakayemdhalilisha muislam,Allah naye atamdhalilisha siku ya Malipo”[bukhari] Ni wahn inayowazuia watawala katika ulimwengu wa kiislam kunyoosha kidole ili kusaidia na kulinda heshima ya mwanamke wa kiislam,si Aafia tu bali ni maelfu ya waislam wakishikiliwa katika gereza la Guantanamo,Bagram na utekaji wa kisiri ufanywao na CIA na mawakala wake.Wakati mtume(s.a.w) atuambia: “Hakika ni faradhi kwa waislam kuwaokoa mateka wao au kuwalipia fidia(ransom) zao(ili waachiwe huru)”
Ni wahn inayowafanya watawala katika ulimwengu wa kiislam kuwakamata,kuwafunga,kuwatesa na kuwadhalilisha mamia ya waislam wa kweli katika magereza yao.Hisham bin Hakeem alisema: “Nilimshuhudia mtume wa mwenyezimungu(s.a.w) akisema,Allah atawaadhibu wote wanaowatesa watu duniani”[Muslim] Lazima tukumbuke kuwa sio sisi tuliokuwa duni na wanyonge namna hii katu.Wakati Utawala wa kiislam ulipokuwepo hapo nyuma,heshima ya mwanamke ililindwa na wafungwa wa kiislam waliachwa huru.Wakati wa mtume(s.a.w) mfua dhahabu mmoja wa kiyahudi wa Banu Qaynuqa alijaribu kuichezea heshima ya mwanamke kwa kumvuta ncha ya nguo yake na kusababisha sehemu yake ya mwili binafsi kuwa wazi bila ya nguo,Muislam mmoja aliyeshuhudia tukio hilo alimuua yule myahudi.Mayahudi nao kwa kulipa kisasi walimuua muislam Yule.Familia ya muislam Yule iliwaita waislam kutoa msaada na mtume(s.a.w) alituma jeshi dhidi ya mayahudi hao na hatimaye baada ya siku 15 waliweza kuwafukuza kabisa kabila la mayahudi hao katika mji wa madina.
Hadithi maarufu ya mwanamke wa kiislam aliyetekwa na warumi na kupelekwa mahali paitwapo ‘Amuriyyah inasimulia kuwa,mudhui si kuwa alikamatwa tu bali aliteswa na kudhalilishwa vya kutosha.Kwa hofu kubwa ya kuwepo peke yake alipiga kelele na kuita jina la Khalifah,[Yaa Mu’tasim]! Ooh! Mu’tasim!!!.Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo alikimbia kwenda kwa khalifah na kumueleza kilichotokea,wakati Khalifah aliposikia kilio cha mwanamke huyu akaitikia kwa ushujaa,uhodari na ushupavu…”Labaik,nimesikia wito wako….”.Alindaa jeshi kubwa kwa ajili ya vita ili kwenda kumuokoa mwanamke huyu.Jeshi la Mu’tasim liliwashinda maadui na kuingia ‘Amuriyyah.Baada ya kuivunja ngome ya maadui hao,walikwenda kumchukua mwanamke huyo na kumuacha huru.
Khalifah Umar bin Abdul-Aziz alituma barua kwa wafungwa wa kivita(POW-prisoners of war) wa kiislam nchini Costantinopole,aliwaambia hivi:

“Msifikiri kuwa nyie ni wafungwa,mpo katika njia ya Allah.Ningependa mutambue kuwa,kila nitoapo kitu kwa waislam basi natoa zaidi kwenye familia zenu.Na nimetuma zaidi na zaidi dinari 5 kwa kila mmoja wenu hata kama akichukua huyo dikteta wa warumi,nitatuma zaidi na zaidi ili kuwahakikishia usalama wenu na muachiwe huru bila kujali gharama.Hivyo furahini,Assalaam alaykum…”

Enyi Amerika na washirika wake! Leo munawauwa wanaume,wanawake na watoto wetu;mnawatesa,kuwafunga,kuwadhlilisha na kupora rasilimali zetu.Lakini yapaswa mutambue kuwa hii ni hali ya muda mfupi,mwamko wa kiislam unanyanyuka na Wahn polepole inayeyuka kupitia maingiliano ya fikra imara ya kiislam.Kumbukeni swali hili ya kwamba
“Ni kwanini mulizindua vita dhidi ya ugaidi hali ya kuwa dhamira yenu ni uislam,na kutumia mabilioni ya pesa kuzichukua nchi zetu?” Wakati wa ushindi wa Allah utakapofika na ardhi za kiislam kuungana chini ya kivuli kimoja cha Khalifah,ambaye yeye ndiye mlezi wetu katika mambo yote msingi kiuchumi,kisiasa,kijamii na katika nguvu za kijeshi wafungwa wote wa kiislam wataachwa huru na heshima ya mwanamke itarejea na kulindwa.

وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَـكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لاَ يَعْلَمُونَ
Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.[TMQ 12:21]