CHIMBUKO LA VYAMA VINGI NDANI YA MFUMO WA KIDEMOKRASIA
Na Farijala malid
Bismillah-Ar-rahaman
Kikawaida kwa kila zama,fikira katika ulimwengu ina chimbuko lake ima chimbuko hilo litoke kwa mwenyezi mungu au kwa mwanadamu.Takribani miaka 100;{karne moja} katika umma huu waliishi nje ya fikira ambayo chimbiko lake ni Mwenyezi Mungu yaani mfumo wa Uislam ambao umeletwa kwa njia ya wahyi kutoka kwa Allah na mwalimu wa mfumo huu ni Bw. Mtume wetu Muhammad (saw) ambaye kwetu sisi kwake ndio kiogozo kwetu cha kupata jibu sahihi na hiyo ndio njia ya haki, fikira sahihi na ndio mfumo wetu wa maisha.
Kama nilivyotangulia kusema kuwa leo tunatakribani karne moja miaka karibu mia moja tangu iangushwe Dola ya Kiislamu katika ramani ya dunia.Ama tukirudi kwenye mada ya vyama vingi katika Demokrasia;ambayo leo hii tunaiiishi ndani ya duara na chini ya misingi ya demokrasia .Ama kwa hakika leo tunaishi kwenye kadhia kubwa na msiba endelevu,ukiwemo uchumi,ukabila ukosefu wa ajira na kupanuka pengo la umasikini .Na hii inatokana na mfumo mbaya wakiasilimali ilio tabikisha nidhamu mbovu ya demokrasia.Naam katika demokrasia vipi wao walianzisha vyama vingi.Wasomi wa fikira hii waliutizama mujitamaa ule mkusanyiko wake wakafahamu kwamba ndani wanadini tofauti,rai,maslahi na mahitaji ,mazingira ya maisha yao pia ni tofauti, kwa hali hii wakawa ni lazima wawe na vikundi ili waweze kufikia kwenye mahitaji yao na hivi ndivyo vikazuka vyama katika mujtamaa ambavyo mwakilishi ni katika viongozi wa chama ;harakati au mungano na nilazima vitambuliwe kisiasa na baya zaidi vyama hivi vina kubali dini zote ni sawa mbele ya Allah taala bali unalazimishwa kukubali kwamba watu wote wana abudu mungu mmoja na hii ni ajenda mbaya kabisa katika Uislamu;Licha ya kwamba ajenda yao inateganisha dini na siasa;ambayo siasa ndio njia ya kumleta huyu mwanadamu imam awe karibu na mola wake na kupitia siasa anaweza akawa mbali vile vile na mola wake.Hivyo basi wakafunga milango ya kutosimama chochote juu ya misingi ya dini au kinyume na fikira yao ya kirasilimali.Na hapo ndipo hasa palipozaliwa neno siasa kali,makundi ya kigaidi,sasa hivi uchochezi au msaliti wa Amani.Dira hino ikaweza kudhibiti mpanuko wa kifikra kwa umma na hata yale makundi yanayo jiita makundi ya Dini yamejifunga ndani ya nyororo hino chini ya hifadhi ya serikali zao za kitwaghuti.
Enyi watu ,Hakika Democrasia ni mwito mbaya sana mbele ya mwenyezi mungu kwani unahalalisha yale mwenyezi mungu alioyakataza zamani sana .Takribani miaka 1500 Hijira hadi leo bado mwanadamu huyu kishipa amekazana kupigia debe ushoga riba na kusagana ;MUNGU Awalaani wale wanaoitikadi kwamba Democrasia tosha ,bali sisi tunasema uislaamu tosha ; Ama kutokana na matatizo mengi duniani ni wazi kwamba Democrasia imeshindwa na uongozi jumla sio Ulaya wala America sio bara Arabu, India, uchina wala Africa kote ni shida Tupu,imma vita vya uchochezi wao,Ama sababisho la umasikini kutoka kwao.Inshallah uislaamu haujakataza vyama vingi lakini lazima vijiunge na ageeda yao tutakuja kusoma nakala nyengine .Wabillah taufiq.
No comments:
Post a Comment