KWA HABARI NA UCHAMBUZI WA UHAKIKA,KITAIFA NA KIMATAIFA,USIKOSE KUTEMBELEA BLOG HII.

Friday, August 14, 2015

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU TANZANIA

MGONGANO KATI YA UINGEREZA NA MAREKANI WAZIDI KUPAMBA MOTO
Na Ahmad Ali
Aliyekuwa mwana CCM mkongwe Edward Lowasa ndieatakaepeperusha bendera ya UKAWA kupitia chama cha Chadema katika kinyang’anyiro cha uraisi mwezi wa oktoba2015.
Chama pinzani Chadema kimebariki mapokezi ya Edward Lowasa kutokea CCM na kumpatia fursa ya kugombea uraisi kupitia chama hicho, na hatimae UKAWA kutia saini ya makubaliano hayo. Kejeli na kashfa za ufisadi ambazo upinzani walikuwa wakizitoa dhidi ya Lowasa kumbe ilikuwa ni debe tupu bila ya kuwa na ukweli wowote. Na huu ndio uhalisia wa demokrasia.
Baada ya uteuziwaCCM uliofuatiliziwa na kumpatamgombea uraisi kupitia chama hicho, ambapomatokeo yakeyaliwastaajabisha wengi katika chama tawala pamoja na upinzani,kufuatia John Magufuli kuibuka mshindi wakupeperusha bendera ya CCM katika kinyang’anyiro cha urais mwezioktoba Huku matarajio ya wengi yakidharauliwa na kupuuzwa kwa kiasi kikubwakatika uteuzi huo mpaka kupelekea baadhi ya wanachama wa CCM kurudisha kadi na kujitoa moja kwa moja ndani ya chama. Lowasa na Benard Membendioyaliyokuwa matarajio ya wengi katikamchuano wa kinyang’anyiro cha uraisi kwa kupitia tiketi ya CCM.
Matarajio haya ya wengi chini ya kisingizio cha demokrasia yalimalizwa na kusambaratishwa bila huruma kwa nguvu na mabavu.Wengiwalishindwa kuelewa kwamba ubepari au maslahi ya kiuchumi ndio yanayo kuwa mbele kuliko maslahi ya kisiasa au kidemokrasia. Kipimo cha maamuzi ya kufanya jambo au kuachakufanya ni faida na hasara , hii ni kwa mujibu wa mfumo huu mchafu wa kidemokrasia. Hivyo ni ngumu kusikilizwa maamuzi ya wengi ikiwaitasababisha kupotea kwa maslahi ya mabwana wakubwa wakoloni pamoja na vibaraka wao.
Mtikisiko wa uteuzindani ya CCM ulikuwa ni wa kukata na shoka baina ya kambi mbili. Kambi ya Marekani na kambi ya Mwingireza. Na hizi ndio kambi mbili kuu zinazoikondesha CCM, na huu ndio mpasuko wa kikweli ndani ya CCM.
Na mpaka sasa kambi ya Mwamerika ndio kambi yenyemakali na ndio  iliyoibuka na ushindi ndani ya uteuzihuo na kumuacha Mwingereza kwenye mataa na mipango yake mbadala. Kambi ya Mwamerika imefanikiwa kushinda katika chaguzi hizo licha ya kuwa makusudio yake hayakuwa kwa John Magufuli , lakini imekuwa hivyo kutokana na mipango na mashambulizi makali kutoka kambi ya Mwingereza ambayo ilijipanga kisawasawa kuhakikisha koloni linarudi kwa bwana mkubwa wa asili  Mwingereza, kwani hapo mwanzo lilikuwa mikononi mwake lakini  Mwamerikaakamfanyia mapinduzi ya kisiasa na kulitia mikononi mwake.
Mwingereza ameshindwa kulirudisha koloni lake la asili kwa kumtumia Lowasa ndani ya CCM. Lakini bado hajakata tamaa anajaribu kuitupa tena karata yake hii ndani ya Chadema kwa jahazi la UKAWA kwa kumtumia mtuwake yuleyule Edward Lowasa. Na hii ni kutokana na kuelewa Mwingereza kwambamtuwake huyu anavyokubalika katika jamii, na kuona matarajio ya karibu katika kurejesha koloni lake.
Chadema ambacho ni chama chaMwingereza kimempokea mwanakambi mwenzao Edward Lowasa na kumvisha joho la kugombea urais bila hata ya kuona haya kwa kejeli na kashafa za ufisadi walizokuwa wakimshutumu nazoawali kwa siri na kwa dhahiri. Vinywa vyao vimefyata kabisa ,haya na fedheha zimewafika kwa sababu ya maslahi ya urais 10/2015. Hichi kipimo cha kimaslahi ndicho watakachoendeleanacho mpaka hata itakapo hakikishika ndoto yao ya Urais.
Edward Lowasa aliyekuwa Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya kwanza ya Rais Kikwete , mnamo mwezi februari/2008 alijiuzulu rasmi kwa kulazimishwa kuachia ngazi ya kiti cha uwaziri mkuu kuinusuru serikali ya Kikwete kufuatia kashfa ya sakata la Richmond. Hakika ya mambo ni kwamba huu ulikuwa usaliti wa wazi dhidi ya Lowasa. Nakuanzia hapo karata hii ya mwingereza ilielewa rasmi kwamba imeshasalitiwa dhidi ya mipango ya kuwa raisi katika awamu ijayo. Kutokea hapo na kuendelea mpaka sasa takriban miaka sita Lowasa alikuwa katika maandalizi mazito ya ndani ya chama na nje ya chama kwaajili ya kampeni ya uraisi mwaka wa2015. Sio hali ya kushangaza hata kidogo kuonekana mtu huyu akipendwa na wengi, kwa kuwa ametumia miaka mingi kufanya kampeni tena huku akishirikiana nabaadhiya wakongwe wa chama cha CCM kama vile akina Kingunge nk. Hivyo kama sio kutumika mabavu katika uteuzi uliofanyika ndani ya CCM basi Lowasa leo angekuwa mpeperushaji wa bendera ya CCM katika kuwania uraisi mwezi oktoba2015.
Zimetumika nguvu nyingi mno zilizofuatiliziwa na mikakati ya hali ya juu katika kumtengeneza na kumnadi Lowasa kwa uraisi mwaka 2015 kupitia teketi ya CCM. Lakini kwa bahati mbaya matarajio hayakuwa.
Hatahivyo,Mwingereza hayuko tayari kuona nguvu zake hizi zikipotea bure bila mafanikio yoyote, na badala yake ameamua kuitupa tena uwanjani karata yake hii kupitia chama chake cha kikoloni cha Chadema na hatimae kupeperusha bendera ya UKAWA.
CUF ndani ya ndoa ya UKAWA ni chama kilichosimama kwa ajili ya kuchunga maslahi ya Mwamerika, chama hichi kamakilivy CCM kipo nyuma ya Mwamerika , kikifanya kazi na Chadema bega kwa bega ili kuchunguza mikakati yote ya Mwingereza inayopangwa kupitia Chadema.
Mwamerika anapanga namna ya kulidhibiti koloni lake na huku Mwingereza anapanga namna ya kulirudisha koloni lakelaasili mikononi mwake. Hakika ya mambo ni kwamba huu ni mpambano mkali wa wakisiasa wa kukatana shoka kati ya Marekani Uingereza.
Mazingatio
Wakati haya yote yakijiri Umma wa Kiislamu umejikuta ukiwa mnyonge ukiburuzwa tu huku na kule kana kwamba ni mtoto yatima aliefiwa na babaakabaki mwenye kutanga tanga tu. Umma wa Kiislaamu umebakia kuchezewa shere na kudanganywa kama watoto wadogo. Waliambiwa wapige kura ya maslahi katika chaguzi zilizopita na wakapiga ‘kula’ ya maslahi. Matokeo yake baadhi ya mashekhe binafsi yalivimba matumbo yao kwa maslahi yao binafsi, wakafungua taasisi zao za kibiashara binafs,i na baadhi wamevurumishwa magerezani na wale wale waliowapigia kura hiyo hiyo ya maslahi. 
Kwahivyo,Ummabadoupo katika machungu na maumivu yapo pale pale. Bado haujapata kuona kwa jicho la wazi na kufunguka akili zao ili zipate kuona uharamu na uchafu wa kushiriki michezo hii ya kiulaghai inayofanywa na wamagharibi kupitia kichaka cha demokrasia.
Misibahiinibaada ya kuanguka kwa Dola ya Kiislaam (khilafah Othmaaniyya) tangumwaka 1924 ambapoUmma wa Kiislaamu umezama kwenye shimo lakiza kinene ukakosa wa kuwakinga dhidiya dhiki, dhulma,uonevu na mateso kutoka kwa makafiri na vibaraka wao.
Lakini kwa Waislaamu wenyekujitambua, tunaamini kuwa hali hii inamwisho kwa uwezo waAllah Taala. Kwani kila lililo na mwanzo halikosi mwisho.Namwisho wa dhulma hizi ni pale itakapo rejeatena dola ya Kiislamu ya Khilafa inshallah , kama vile alivyobashiri Rasuli s.a.w kwa kauli yake aliposema: 
“ Kisha itarudi tena khilafah kwa njia ya Utume”

No comments: