KWA HABARI NA UCHAMBUZI WA UHAKIKA,KITAIFA NA KIMATAIFA,USIKOSE KUTEMBELEA BLOG HII.

Friday, December 4, 2015

KOMBA NI WALE WALE,LAKINI MISITU SI YA KALE

                              
Tangu wakoloni wa kimagharibi kuvamia biladi za Kiislam na bara  la Afrika hasa kuanzia mwaka 1881 hadi 1914,na kuendeleza hadi leo,njama za kusambaza mfumo wao wa kibepari na nidhamu yake ya demokrasia,uliojengwa juu ya akida potovu ya kutenganisha dini na siasa na wenye kuwapeleka watu,kwa kipimo cha maslah kama kipimo cha kutenda au kuacha.
Kumekuwepo na uvamizi,wizi,utapeli na uporaji wa malighafi kama alivyowapaka mafuta kwa mgongo wa chupa,vibaraka watawala wa Afrika,kwa kutoa jongoo mchuzi,

"Africa is a victim.Africa has always been exploited by other powers···There are some countries that only want the great resources of Africa.But they dont think about developing the countries nor creating jobs.Africa is a martyr,a martyr of the exploitation of history!"The Daily Nation.

Kama iblis,amesema kweli papa Francis,japo yeye mwenyewe muongo.Kama kweli apinga ukoloni,asingehubiri akida ya kikoloni kutofautisha dini na maisha,kuilingania na kuwaita Waislam kupigania  fikra na thaqafa za kibepari kama dini mseto,uhuru wa kuabudu,kutofautisha dini na maisha(secularism) na dini za Ibrahim.Bali wakatholiki ndio washirika wakuu,waliowakubalia wanafalsafa wa kibepari demokrasia,kupiga vita Ahkam za Allah Taalah zama za The French Revolution 1789.
Kando na kuwatumikia kuvamia biladi za Kiislam na Afrika,kiasi cha kupatikana msemo,"Where The Cross Went,The Flag Followed".Mpaka kesho,kanisa latumiwa na wakoloni mamboleo,ktk njama zile zile za jadi walizozitumia dhidi ya Waislam.
Njama hizo,zimeshuhudia kuwepo kwa wizi,uvamizi,uporaji wa rasilimali za biladi za Kiislam na bara la Afrika.Huku mabepari wakibatiza unyonyaji huo,majina kama Scramble For Africa,Conquest Of Africa na Partition Of Africa.Wakitumia sera tatu kuu walizozitumia,kumakinisha fikra na thaqafa zao chafu,na kufaulu kupenyeza sumu sehemu za mbali,ambazo hata majeshi yao hayakutia guu.
Wakoloni wa kijerumani,walizua mbinu ya kuvamia ilopewa jina ASSOCIATION POLICY.Mbinu hii,waliitumia kwa kujifanya wema wenye kujali maslahi ya Ummah,kwa kushirikiana nao.Japo walikuwa mbweha,walojigubika gubi gubi ngozi ya kondoo.Wakoloni mabepari wa kijerumani,waliitumia mbinu hii kila sehemu waliyokwenda kuiba mali za wakazi hasa Tanganyika.
Haki daima dawama yaelea,wala haitozama.Wakazi wakagundua njama hii walipoona wanyimwa haki zao hata kupanda pamba na kutangaza vita dhidi ya wajerumani,na kutokea mapigano yaliyopewa jina Maji Maji Rebellion yaliyoongozwa na Tinjekitile Ngwale mwaka wa 1905-1907 na kupelekea wakazi wa Tanganyika kufa kwa njaa kwa sababu ya mbinu ya kuharibu ardhi na mimea (schorched earth policy) ilotumiwa na Gustav Adolf von Götzen.
Wafaransa wakaja na yao.Waliyoiita ASSIMILATION,ambayo waliitumia kuwalazimisha watu hasa Waislam wenye thaqafa,fikra,mila desturi na mfumo tofauti,kuacha mfumo, mila,desturi,fikra na thaqafa zao na kufuata zile zao za kikoloni.Yeyoye aliyekataa au kupinga,aliteswa,akatengwa,kunyimwa haki zao msingi na hata kuuliwa.Mbinu hii,kando na kumakinisha ukoloni wa dini ya kibepari-demokrasia,ulieneza fikra,thaqafa,mila,desturi na akhlaq potovu kwa kutumia baadhi ya watu walioikubali kwa kuhadaiwa kupewa haki sawa na wananchi wa France mwaka wa 1845.
Mnamo 27-4-1848,kulipitishwa kanuni Jijini Paris kuwapaka wanja wakazi wa maeneo haya kufuatia mapinduzi ya Ufaransa.Japo kufikia tarehe 2-4-1852,wakaachwa mataani na.kuondolewa usawa huo.Na kufikia 1945,ikawa dhahiri shahiri hakuna usawa wowote baina ya Wafaransa na wengine.
Wafaransa walitumia mbinu hii kuipanua dola yao.Sehemu fulani za Senegal kama Dakar,Rufisque,Gorée na Saint Louis zikamizwa na Ufaransa kwa mbinu hii.
Wakoloni wa Kiingereza,wakaja na mbinu yao.Lengo likiwa lile lile moja.Kuvamia biladi za Kiislam na bara la Africa.Nao mbinu yao,ilitofautiana na wengine.Mbinu yao ikiitwa DIVIDE AND RULE.Mbinu hii ilitumika kuwagawa wakazi Kijiografia,Kikabila,kirangi,kimadhab,kidini na kuwaacha wakitazamana kwa jicho la uadui na uhasama usio na mfano.Na kuonyeshwa kuwa abadan hawawezi kuishi pamoja.Hivyo kuwapa wakoloni mabepari afueni.
Kwani wakazi na Waislam,walishuhulishwa kujiangalia wao kwa wao kama maadui,na huku wakiwaacha wao salama salimini.Kwa mfano,leo Waislam huteta,kutukanana,kuaibishana kwa tofauti za kijiografia,kikabila,rangi,nasaba au madhab.Na kuona wasio kuwa Waislam au wa mkao na jinsia yao,kuwa maadui waovu wasioweza kutangamana.Wasiokuwa Waislam wakiwemo mayahudi na manaswara,waliishi chini ya Khilafah kama ma-dhimmi bila wasi wasi.Japo madhab wameyarithi.Na hao walotuletea,wote waliishi pamoja chini ya kivuli cha Khilafah.Wakiheshiminiana, kutangamana na kufanya biashara pamoja bila ya uhasama.Mbinu za komba wa kale,leo zatumika kuwaghilibu wakazi wa misitu mipya.
Hapa yadhihirika kuwa,wakoloni washabaini tangu shina hadi kilele,kuwa kifo cha mfumo wao kimewadia.Na wamejaribu kila mbinu kuupa life support wakaambulia patupu.Hivyo,waomba msaada kwa watu wasio na ufahamu wa kina juu ya mfumo na siasa zao,na mbinu zao chafu wanazozitumia kuulinda,ili wawape msaada wa kuupa uhai japo kwa muda.Kifo cha kima,miti yote huteleza.
Naam,wamefaulu kuwapata baadhi wenye kuwasaidia kwa kuendesha gurudumu la ubepari.Ima kwa kuleta utesi na migawanyiko ya kimadhab,kikabila,kirangi,kinasaba,kidini,kizalendo ili Uislam uonekane hauwezi kuwaunganisha raia.
Lakini sasa wengi waona uovu wa mfumo wao.Si Waislam tu hata wao wenyewe.Murtada Mbaraka (Barack) Hussein Obama,aliwaonya Waislam Malaysia kuhusu kufuata nyayo za America yenye kufuata ubepari.
Rais Evo Manuel wa Bolivia,akapasua mbarika kwa walimwengu wote aliposema kuufuata ubepari ni KUANGAMIA,"If we continue on the path trod by CAPITISM, we are condemned to disappear!" The Daily Nation.

                                                    

                                    "Na karibuni atakupa mola wako,na utaridhika(utafurahi)"
                                                                        (TMQ Dhuhaa)

No comments: