Na Shabani Mwalimu
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani papa Francis yuko barani Afrika kwa
ziara ya siku tano. Akiwa nchini Kenya, papa amefanya mazungumzo na
viongozi wa viongozi kidini kuhusu umoja wa imani tofauti za kidini.
Akapinga ugaidi na kutoa mwito kwa viongozi wa kisiasa kuondosha uhasama
wa kisiasa badali yake wajenge matangamano na amani. Mwito huo pia
ataukariri akiwa nchini Uganda. Kiongozi huyo atamalizia ziara yake
katika Jamhuri ya Afrika ya kati, nchi inayogubikwa na vita baina ya
wanajeshi wa serikali wa kikristo na kikundi cha Waislamu cha Seleka na
kupelekea Waislamu wengi kuuliwa kinyama.
Harakati ya Kiislamu ya Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki ingependa kuizungumzia ziara hii kwa kusema yafuatayo:
Mazungumzo baina ya imani tofauti za kidini ni fikra ya kimagharibi na wala haina asili ya Uislamu. Fikra hii inatokamana na itikadi ya kiilmaniyyaa ya kutenganisha Dini na maisha na kuwapa wanadamu mamlaka ya kutunga kanuni badali ya sheria za MwenyeziMungu. Fikra hii chafu ni silaha wanayoitumia wamagharibi kupenyeza fahamu na fikra za kimatata kwa Uislamu. Lengo hasa ni kuwataka Waislamu waachane na Uislamu wao aliokuja nao Mtume Muhammad SAAW) badali yake wafuate dini mpya ya kiilmaniyya. Sisi hatushangazwi na Papa kuongoza mazungumzo haya kwani yeye mwenyewe na waliomtangulia awali amekubali kumeza sumu ya ilmaniyya iliomlevya hadi kufikia kuwatungia sheria wafuasi wake. Kwa hakika usekula umeathiri kanisa lake hadi baadhi ya mapadri wake kufikia kiwango cha kujitangaza hadharani kuwa ni mashoga! Kinachotusikitisha sisi ni kuwaona baadhi ya viongozi wa Kiislamu- Mola awaongoze wameingizwa kwenye jukwaa hili la kuwafitinisha Waislamu kwenye dini yao kwa kisingizio cha mazungumzo baina dini.
Uhasama wa kidini baina ya jamii, hausababishwi na Uislamu bali umetokamana na mfumo wa kikoloni wa kibepari na serikali zake zenye kuchochea mabaya haya. Hapa Kenya, jamii ya Kiislamu haina historia ya kulazimisha wakristo misimamo ya Uislamu bali kanisa ndilo limekuwa likihubiri chuki dhidi ya mahakama za kadhi na kupiga vita vazi la hijab kwa wanafunzi wa kike wa Kiislamu. Na sisi twajua kuwa Papa Francis anasahau ama kujisahaulisha kuwa viongozi wa kidemokrasia ndio hupachikiza chuki za kikabila na kimaeneo zinazogeuza Afrika bali dunia kuwa uwanja wa vita. Lawama za michafuko yote na mifarakano zinastahiki kutupiwa mfumo wa kimagharibi na siasa yake ya kidemokrasoa na wala sio Uislamu. Licha ya wakatoliki licha ya kuitikia mwito wa papa Benedikti kupigana na Waislamu kwenye vita vya mslaba karne ya kumi, lakini walipokuwa chini ya utawala wa Kiislamu wa Khilafah hawakulazimishwa kubadilisha misimamo yao ke ya kidini japo inagongana na Uislamu.
Ama kukashifu ugaidi, tungempongeza papa lau kwenye ziara yake ya hivi majuzi huko Marekani, angeikashifu dola hiyo na kuitaka itoe wanajeshi mashariki ya kati wanaotekeleza ugaidi wa kutisha! Bila shaka uvamizi huu ndio chanzo cha kuzuka Kwa kile akiitacho ugaidi. Sisi twabaini kuwa baada ya Amerika kufaulu kuangamiza muungano wa kisoviet, hatimaye kuanguka kwa ujamaa/ukomonisti mwishoni mwa miaka ya thamanini karne iliopita, majivuno yake Marekani yamezidi na sasa anaelekeza vita dhidi ya Uislamu ambao hivi karibuni utasimama na kuongoza dunia. Hivyo Amerika imeajiri serikali zote duniani yakiwemo mashirika kadhaa kusaidia kujenga rai jumla dhidi ya Uislamu.
Mwisho twasema ziara hii ya Papa haikuwa ila kujaribu kuduwaza watu waendelee kuwa mateka wa mfumo muovu wa kirasilimali na itikadi yake ya kipagani. Wakati huo huo ikitupia lawama Uislamu na Waislamu ili wasiweze kuendelea kuulingana kama mfumo kamili wa kimaisha ulio na uwezo wa kukomboa walimwengu wote.
Kumb: 02/1437 16 Swafar,1437 Hijri 28-11-2015
Simu: +254 720597841 / +254 789 574 608
Pepe: abuhusna84@yahoo.com

No comments:
Post a Comment