Huo ni waraka ulioandaliwa na Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) uliokusudiwa kusambazwa kuanzia tarehe 30/09/2010 kwa maimamu wa misikiti mbali mbali Zanzibar kuhusiana na Uchaguzi Mkuu uliopita wa mwaka 2010. Amiri wa JUMAZA wakati ule alikuwa Amir Farid na Katibu Mtendaji ni Muhiddin Zubeir
Katika nukta ya 4 Waraka huo ulisomeka hivi:
“Taasisi za Kiislamu zinawahimiza Waislamu kushiriki kikamilifu katika zoezi la kupiga kura kwa amani na utulivu na kupuuza wito wa Jumuiya ya Hizb ut-Tahrir unaowataka wasusie kupiga kura katika uchaguzi mkuu. Aidha, Waislamu wanatakiwa kutowaruhusu wanachama wa Jumuiya hii kutumia misikiti kuwachanganya Waislamu katika kipindi hiki muhimu katika historia ya nchi yetu."
Kabla ya kusambazwa waraka huo, tarehe 28/09/2010 mashababu wa Hizb ut
Tahrir ndani ya Zanzibar walitoa waraka wa majibu kwa waraka huo.
Katika nukta ya sita ya majibu hayo ilisomeka hivi:
“Mnatoa mwito ili demokrasia ishike mizizi na Sharia za Allah Taala zitupiliwe mbali? Jee hamjui kwamba ‘kila chenye kupelekea katika haramu nacho ni haramu’? Huu kamwe si mwito wenu, wala nyinyi hamna kauli juu ya vyama vya kidemokrasia kama mnavyojikweza na kujipendekeza, na si muda mrefu mtaachwa mkono. Ikiwa wanademokrasia husalitiana wao kwao wao ambao vipimo vyao ni sawa. Jee mtasalimika nyie?
Allah Taala Awape faraja ndugu zetu na tawfiq ya kutanabahi na kutubu -Amiin

No comments:
Post a Comment