HAIPUNGUZWI GHARAMA KWA KUPUNGUZA IDADI YA WATU BALI ZITAPUNGUZWA AU KUONDOLEWA GHARAMA KABISA KWA KUUONDOA UBEPARI.
Na Abdulrasheed Abdullah
Mabepari huwa na kanuni ya kuwapa watu ufahamu wa kioo,yaani
hulizungumzia jambo kwa sura ya kulia wakati kiuhalisia lipo
kushoto.Kipimo kikubwa cha ubepari ni maslahi,kinachomsukuma mtu kufanya
jambo ingawaje ukikitazama kwa jicho angavu utaona namna gani
kilivyofeli.Mfano,wakati watu wa Uropa wanaelekea kwenye mapinduzi ya viwanda,ilidhaniwa kwamba uzalishaji utaongezeka sambamba na gharama kupungua ikiwa kutapunguzwa gharama za uzalishaji zinazosababishwa hasa na utegemeaji wa nguvu za watu(labour) katika uzalishaji.Mbinu hii ya utumiaji wa nguvukazi(labour) sana kuliko mashine hujulikana kama labour intensive,
Hivyo wakapendekeza kutoitegemea sana mbinu hii ya nguvu kwenye uzalishaji na badala yake itumike mbinu mpya ya uzalishaji ambayo ni capital intensive ambapo mashine ndio huwa na nafasi kubwa kuliko binadamu.Matokeo hasi ya mbinu hii ni kuzidi kuongezeka tatizo la ajira ulimwenguni,watu milioni 10 wanaweza kukosa kazi kutokana na kutumiwa mashine moja tu kwenye uzalishaji.
Baada ya kushindwa kutatua tatizo la ajira ulimwenguni na kutaka kudhibiti mwamko wa watu ulimwenguni ili wasije wakachukua maamuzi ya kutaka kupora mali zinazomilikiwa na watu wachache(warasilimali),Program mpya ikaanzishwa ya kudhibiti vizazi ambapo mbinu nyingi zimetumika ndani yake kama Family planning,uzalishaji wa vimelea vya magonjwa,utengenezaji wa bidhaa zenye sumu,kuchochea vita na uhasama n.k
Yote haya wameyaleta ili kuweza kulinda maslahi yao yaani kupunguza #Gharama.
Ajabu! mpaka leo wanaovikwa taji la usomi wanaendelea kufikiri na kudhania ndani ya mipaka ya duara waliolichora mabepari hawa wa Uropa,kuwa gharama hupungua kwa kupunguza idadi ya watu...
Kihakika MAGUFULI naye atashindwa kupunguza gharama kupitia njia hii ya kupunguza idadi ya mawaziri serikalini.
Ni jambo dogo tu yafaa kujiuliza,kwani gharama za elimu,afya,usafiri,umeme, unga,mchele,maharage,sukari,mafuta na bidhaa zote zinazozalishwa ndani ya nchi zimepanda kwa sababu ya kuwepo na mawaziri wengi?
Ukweli ni huu,kupunguza idadi ya mawaziri sio ndio njia ya kupunguza gharama za maisha kwa ummah unaoutawala.Hivi kuna nchi angalau moja imewahi kushuka deni la taifa mpaka kufikia 0%? na kama hakuna,je sababu wana mawaziri wengi?
Nahofia kadri muda utakapozidi kwenda bila ya kuuleta mfumo mbadala,linaweza likaletwa wazo la kutumia obot kuongoza nchi ili kupunguza gharama maana hakutokuwa na haja ya kumlipa mshahara....

No comments:
Post a Comment