KWA HABARI NA UCHAMBUZI WA UHAKIKA,KITAIFA NA KIMATAIFA,USIKOSE KUTEMBELEA BLOG HII.

Sunday, January 31, 2016


KADHIA YA MARUDIO YA UCHAGUZI NCHINI ZANZIBAR: MASSOUD MSELEM-Mwakilishi kwa vyombo vya habari wa Hizb ut tahrir Afrika Mashariki





MASOUD MSELLEM, Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Afrika Mashariki. Akifanya uchambuzi wa "Kadhia ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar" unaotarajiwa kurudiwa tarehe 20 Machi, 2016 Visiwani humo.
Posted by Hizb ut-Tahrir East Africa on Tuesday, 26 January 2016

Wednesday, December 30, 2015

"MWAKA MPYA" MBINU YA WANADEMOKRASIA KUSAHAULISHA MALENGO YA UMRI .

 
"MWAKA MPYA" MBINU YA WANADEMOKRASIA KUSAHAULISHA MALENGO YA UMRI .

Hamza S. Sheshe
Mwaka 325 AD Kanisa Katoliki lilifanya mkutano mkuu wa kwanza huko Nicea. Mkutano huu uliitishwa na Mfalme Constantine (mpagani) ili kutuliza hali ya machafuko iliyosababishwa na wakristo waliokuwa wakipinga falsafa ya uungu iliyoasisiwa mwanzoni na Justin Martx, (Yusto). Huu pia ndio mkutano ulioanzisha misingi ya aqeeda ya ukristo wa leo iliyohusisha ‘utatu mtakatifu’, ‘dhambi ya asili’ na kufufuka kwa Yesu. Aidha, ndilo Baraza hili la Nicea lililoweka msingi wa Kalenda iliyokuja kuitwa Kalenda ya Gregorian kwa kulazimisha Wakiristo wote washerehekee Pasaka siku moja. Misimamo ya Baraza la Nicea ilipingwa vikali na baadhi ya Wakiristo ikabidi kanisa kuomba msaada kwa serikali (ya kipagani) isaidie kurejesha amani na utulivu. Katika upinzani huu waliteswa maelfu kama si malaki ya Wakiristo na wengi kuuwawa. Mabaki ya vifaa vya kutesea bado vinapatikana katika jumba la makumbusho huko Rhine, Ujerumani.
Kuanzishwa kwa kalenda ya Miladi ya Papa Gregory XIII lilikuwa ni jaribio la kufanya marekebisho kalenda ya Julian (iliyoanza mwaka 45BC) iliyokuwa ikitumiwa awali. Papa Gregory alisimamia mabadiliko haya, na rasmi katika tarehe 24 Februari 1582 akasaini waraka maalumu unaojulikana kwa jina la “Papal bull’ ili kuimakinisha kalenda hii :http://en.wikipedia.org/wiki/Gregorian_calendar.
Wakatoliki waliikubali kalenda hii kwa kuwa waliamini kwamba dhamira ya Mkutano wa Baraza la Nicea ulioanzisha muundo mpya wa siku ya Pasaka ilikuwa pia kuanzisha kalenda mpya. Japo kwamba lengo la Mkutano lilikuwa ni kupata tarehe maalumu ya kusherehekea Pasaka kwa Wakiristo wote kwa pamoja. Kabla ya hapo Pasaka ilikuwa ikisherehekewa mwezi wa habib ( unavyojulikana katika Bibilia )uliokuwa ukiisabiwa kwa kalenda ya mwezi. Lakini kwa kuwa muandamo wa mwezi hubadilika badilika ndipo Kanisa Katoliki likafanya mabadiliko makubwa ndani ya mwaka 325. Mabadiliko ambayo yalitoa viashiria vya kubadilisha muundo mzima wa kalenda ambao baadae ulikuja kumakinishwa na Papa Greogry wa kumi na tatu.
Hata hivyo baadhi ya makanisa yasiyokubaliana na upapa wa Kikatoliki yalikataa kalenda hii.
Miongoni mwao ni Waporestanti na Kanisa la Orthodox. Mataifa mengine yalianza kuikubali kalenda hii kidogo kidogo, hata Khilafah Uthmaniya ilikubali kuitumia kalenda hii katika miaka ya 1890 wakati wa zama zake za uzorotefu, na kuibakisha kalenda ya Hijiria katika mambo ya kiroho na ibadat tu.Kama vile katika hesabu ya Ramadhani na Hijja. Hii ni baada ya kudorora kwa kiasi kikubwa kwa dola ya Kiislamu, kiasi cha baadhi ya Waislamu hususan wasomi walioathiriwa na fikra za kimagharibi kama vile mhasibu Morali Othman (Msomi wa Kiislamu aliyeathiriwa na umagharibi ) kupendekeza kutupilia mbali kalenda ya Hijiria kwa kudai ina usumbufu katika masuala ya hesabu za kifedha.
Suala la kalenda au kuhesabu siku ni jambo tu la kumuwezesha mwanaadamu kuweka kumbukumbu na malengo yake ya kiutendaji na haliingia katika masuala la kiutawala. Ndio maana, japo kuwa kalenda hii asili ni ya Kanisa katoliki , lakini inafuatwa/adopted na sehemu kubwa ya dunia kama si yote. Pamoja na ukweli kwamba si Ukatoliki unaotawala dunia leo. Na badala yake dunia inatawaliwa na mfumo wa kibepari/kidemokrasia. Kwa kuwa ukiristo kamwe sio mfumo wa kimaisha wenye sifa na uwezo wa kumtawalia mwanaadamu na wala hauna masuluhisho ya mambo ya kimaisha. Bali ni kijidini kinachojumuisha baadhi ya fikra za masuala ya kiroho tu.
Mfumo wa kibepari unazitumia sherehe za mwaka mpya kukuza na kuimarisha fikra zake za ‘uhuru’ kwa kiasi kikubwa na masoko ya kibiashara. Huhamasisha kusherehekea kwa namna tofauti kama kulewa, kuzini, kucheza miziki, kamari, kuleta vurugu nk. Aidha, wanaipotosha na kuidogosha hazina muhimu na yenye thamani ya umri wa mwanaadamu na kupongezana kwa kumaliza mwaka salama usalimini bila ya kuwaonesha watu dira na malengo ya umri huo.
Uislamu ni kinyume na Ubepari/Udemokrasia ambao huwafanya watu kutokujua lengo la kuwepo duniani. Wao huona kila kitu kinaishia hapahapa na hakuna hisabu ya matendo kwa Muumba. Na ndio maana itikadi ya Ubepari/Udemokrasia wao huona kwamba kama Muumba yupo basi baada ya kuumba na kumpa mtu akili amemuachia ajipangie mfumo wake anaoutaka maishani kwa faida na hasara ya mwanaadamu mwenyewe. Wala Muumba hana tena nafasi ya kumhisabu mtu huyu. Aidha, Uislamu kamwe haudandii sherehe zisizokuwa za Kiislamu kwa kuwa tayari una sherehe zake zilizowekwa na sheria.
Badala yake Uislamu umeweka wazi lengo la mwanaadamu katika maisha haya kwamba ni kumtumikia Muumba. Na kila dakika mtu ajihesabu kabla ya kuhesabiwa, sio kwa faida ya kimada bali katika kushikamana na maamrisho ya Muumba. Tathmini hiyo sio baada ya kumalizika mwaka. Bali ni kila dakika na kila siku. Yaani Muislamu ajihesabu kabla ya kuhesabiwa.
Waislamu lazima tukumbuke katika umri huu tuna jukumu la kuongoza ulimwengu:
وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا
“Na vivi hivyo tumekufanyeni umati bora ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe shahidi juu yenu” (TMQ 2:143)
Kwa bahati mbaya leo tunaishi chini ya mfumo wa kikafiri ulimwenguni kote. Licha ya kuwa ni faradhi kwetu kuishi chini ya dola ya Kiislamu ya Khilafah, na ni dhambi kubwa kuishi zaidi ya siku tatu nje ya dola hiyo. Leo ni mwaka wa 88, bado tupo chini ya utwaghuti wa kirasilimali na demokrasia ilhali baadhi bado hawajatanabahi wala kuamka. Kila siku inayopita inakatika sehemu ya umri wetu, tunasonga hatua mbele kuelekea mauti na kuhisabiwa na Allah Taala. Aidha, ni hatua moja nyuma ya muda wa kutekeleza majukumu tuliyofaradhishiwa na Allah SW. Basi jee wakati haujafika wa sisi Waislamu kuamka na kujizatiti katika majukumu yetu?

Friday, December 25, 2015

UISLAMU PEKEE NDIO UNAOJALI FAMILIA

Na Suleiman Abdullah

Tarehe 15 Mei ya kila mwaka imetangazwa ni Siku ya Familia Duniani. Nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa huiadhimisha siku hiyo inayotokana na Tamko la Baraza la Umoja wa Mataifa No. 47/257 la tarehe 20/09/1993. Tamko hilo liliifanya siku hii kuwa maalum kwa ajili ya familia. Nchi zote duniani huiadhimisha siku hii kwa kujadili nafasi ya familia kwenye jamii na maendeleo kwa ujumla.
Cha kushangaza ! wanademokrasia wanaweka Siku ya Familia ilihali nidhamu ya kidemokrasia ndio mdau mkubwa wa kuvunja na kusambaratisha hizo familia. Kwa mfano, Ulaya imefikia mpaka mama na mtoto wanaishi kimkataba. Kwa hakika suala hili ni fedheha kubwa kwa mfumo wa kibepari na nidhamu yake ya kisiasa ya kidemokrasia.

Aidha, tunashuhudia namna fikra za kimaslahi, ukandamizaji wa kiuchumi wa mfumo wa ubepari unavyozipeleka mchamchaka familia kiasi kwamba hazina muda wa kuketi pamoja. Kwa sababu muda mwingi kutumia kazini au mashuleni. Karibuni mbunge Susan Lyimo (Viti maalumu Chadema) alitamka wazi kwamba msongamano wa magari jijini Dar-es Salaam unaanza kuleta migogoro ya ndoa ndani ya familia (Gazeti la Mwananchi. Uk 16. Mei 9, 20014) Kwa kuwa baba muajiriwa na mama nae kutokana na hali ngumu, fikra za kujiongezea, shinikizo la kiuchumi, fikra za uhuru wa mwanamke pia nae muajiriwa, na watoto wanasoma shule ya bweni. Mama akirudi kachoka na baba akirudi kachoka hawana muda wa kukaa pamoja. Na kwa watoto wasiosoma shule ya bweni wakirudi nao pia wana kazi za nyumbani (homework). Ikiwa vikundi hivi vitatu baba, mama na watoto hawana muda wa kuketi pamoja kufurahi na kuchanganyika pamoja kwa ajili ya ustawi wa kifamilia. Vipi tena watakuwa na muda wa kuwatembelea jamaa wengine wa karibu?

Na kwa upande wa fikra ya kimaslahi Ubepari/udemokrasia umeshindwa kuzifanya familia kuwa kitu kimoja. Kwani mfumo huu unalingania kila kitu kupimwa kwa mtazamo wa kimaslahi. Hata kumpenda mama, baba, dada nk. mtu huaangalia kwa jicho la maslahi fulani. Ndio maana ukaona ndugu humpenda dada, kaka au jamaa mwenye uwezo zaidi kifedha kuliko asiyekuwa na uwezo. Au pia wazazi nao humthamini zaidi mtoto mwenye kazi na fedha kuliko aliyekuwa hana kazi na uwezo. Kipimo cha maslahi kimeweza kuvunja na kusambaratisha familia nyingi sana. Tunashuhudia hata hapa petu kila siku familia zinagombana hata kwenye masuala madogo madogo kama mirathi hadi kufikia kutukanana matusi ya nguo na kupigana hadharani bila ya aibu wala fedheha na hatimae kuvunja udugu ambao ni kitu adhimu kutoka kwa Mola wetu Muumba.

Tusisahau pia fikra chafu nidhamu ya kidemokrasia za uhuru (freedoms). Yaani mtu kufanya alitakalo. Hakika ni kioja kikubwa kwa wanademokrasia kumlingania mwanadamu kwamba ana uhuru wa kufanya anavyojisikia. Fikra hizi ndizo zinazozalisha kila aina ya maovu kuanzia uzinifu, ulevi, usagaji, ushoga nk. Na kwa kuwa hawawezi kuyakhalifu yaliyozaliwa na fikra hizo, leo kwa upotofu mkubwa tafsiri ya familia imetanuliwa mpaka kuhusisha watu wa jinsia moja. Yaani kinachoitwa ndoa ya wanawake kwa wanawake na wanaume kwa wanaume. Subhannallah!

Hapana shaka maadhimisho ya Siku ya Familia na mithili yake hayana tija yoyote kwa Umma bali ni michezo ya kimaslahi wanayoiweka mabepari kujiongezea kipato kutokana na maandalizi ya matamasha na maonyesho mbalimbali ambayo bajeti zake hutunisha mifuko yao.

Uislamu ukiwa mfumo wa haki ndio unaojali familia kipindi chote na sio siku moja kwa mwaka. Aidha, umeikunjuwa dhana ya familia kwa upana sio mume, mke, watoto na mbwa wao ! Bali inahusisha jamaa wote, na ni haramu na dhambi kubwa kuwatupa.
Tunaona sera ya Uislamu jinsi gani unavyohimiza kutunza familia na kuiendeleza kupitia maamrisho na makatazo aliyoyaweka Allah Taala kwa viumbe vyake kupitia Mtume( SAAW). Yeye ametuhimiza, kutufundisha na kutushajiisha kutunza familia. Uislamu umetangaza wazi kwamba baba ni mchunga na ataulizwa kwa kile anachokichunga. Kauli hii pekee yatosha kuonyesha jinsi gani mzazi anapotakiwa kuwa karibu na familia yake ili kuipa huduma mbali mbali yakiwemo maadili mema. Na Allah Taala kutoa fursa ya kuoa mke zaidi ya mmoja ni dalili tosha kwamba wanaume wana uwezo wa kutunza familia. Na chini ya kivuli cha dola ya Kiislamu ya Khilafah mazingira ya kutunza na kusimamia familia yatasahilishwa zaidi ili kuhifadhi taasisi hiyo muhimu katika ustawi wa wanadamu

Sunday, December 13, 2015

SHEREHE ZA JAMHURI KENYA NA UHURU WA BENDERA.




Kila mwaka ifikapo mwezi wa disemba tarehe 12,huwa ni siku kuu ya kitaifa nchini Kenya.Siku hio huwa ni kwa minajili ya kuadhimisha siku Kenya ilipokuwa ikingia rasmi kwenye dira ya mfumo wa kikoloni ubepari democrazy, kwa njia ya jamhuri(republicanism).
Jamhuri huwa ni mfumo wa kiutawala wa kibepari wenye kudhamini nyadhifa za serikali kuwa wazi na kugombewa kwa njia ya kura kila baada ya muhula fulani,ikiwa moja ya njia ya kustiri hali ya mfumo wao muovu na pia kumdumisha yule atakae kuibuka mtwiifu kwao kama Yoweri Kaguta Museveni.Licha kuwa mtawala wa kiimlaa kuwakandamiza wapinzani na upinzani wa vyama vingi unao lazimishwa kwengine yeye hana wala hapigwi vita.

Kufuatilia mkutano wa Berlin Conference ulioandaliwa na wakoloni kujigawia ngawira za rasilimali za madola mengine ukiongozwa na Chancellor Otto von Bismarck wa Ujerumani,Kenya iliitwa British East Africa,na kupewa Waingereza kuitawala ambae akaleta walowezi(settlers) wa kizungu kuja kutwaa mashamba ya wenyeji wa Kenya.

Licha ya idadi yao ndogo walowezi hao walikuwa na ushawishi na msemo ktk serikali yao ugenini Kenya.
Huku wenyeji wenye asili ya kiafrika na wahindi,wakiwa hawana hawanani bali hata ardhi zao ziliporwa na wakatimuliwa kama Waislam wanavyofanywa leo Falastin na mayhudi, kubwa isitoshe wenyeji walikuwa wakitozwa ushuru kufanyishwa kazi za sulubu na kulipwa mshahara duni.

Baada ya wakoloni kuchoshwa na sera zao za kuwasimamia wengine moja kwa moja(direct rule),walichochea fikra za uhuru kwa kuamsha hisia za uzalendo na utaifa miongoni mwa wenyeji na walipoweza hata hisia mbovu za ukabila.
Japo raia wa kawaida walihadaiwa ati wapigana na wakoloni ili kuwatimua na kurudisha rasilimali mikononi mwao.
Ukweli ni kuwa wakoloni hawakushindwa kivita wala jambo hili haliingii akilini. Waafrika,wahindi na waarabu walokuwa na silaha duni hafifu zama zile,waweze kushinda jeshi la serikali kuu au wakoloni waliokuwa na ndege ,manuwari,vifaru,bunduki na hata kushiriki vita vikuu duniani.

Ukweli ni kuwa wakoloni walibadilisha sura mpya ya ukoloni,Kutoka ile ya zamani ilokuwa ikitoa hali ya dhati kamili ya uovu wa mfumo wao kutoka kwa wakoloni moja kwa moja hadi hini ya sasa,ambapo nchi hupachikwa vibaraka wenye kuwahudumia wazungu.

Na mapungufu ya mfumo huo yamesitirika kiasi kwani huonekana kama dosari ya viongozi vyama tawala au miuungano ya kisiasa.
Wala sio wakoloni na mfumo wao duni kama ilivyo hali kwa sasa.
Kila mfumo ukionyesha kucha zake mbovubasi viongozi hasa wa upinzani au raia adi wasojua dhati na uhalisia wa mfumo huo hudai kuwa viongozi waliomamlakani,ndio waovu.
Wapinzani huzidisha kutia chumvi ili kutafuta kula huku raia wakitumiwa kama ngazi.
Tujiulize kama si mfumo kuwa ndio shina la matatizo mbona America ishabadili marais na ishapiga kura zaidi ya miaka 200,hadi sasa kuma dosari na mapungufu mengi.
Na kila mgombezi adai sawa wa upinzani au utawala,wadai kuleta islahi na kuondoa shida.

Sera hii mpya ya ukoloni ilimpa Jomo Kenyatta,urais wa kwanza nchini 12:12:1963.Hili halikutokea rahisi bali baada ya kumpika kwa miaka na dahari ktk safari zake za Uingereza.

Hapa Jomo Kenyatta aliibuka kufaa zaidi hivyo ikabidi wamlinde kwa miaka takriban 7 kwa kumueka jela kwa kisingizio ati ni mpinzani wao mbaya,Mau Mau hatari na tishio kwa usalama.
Japo Percy Sillitoe,aliekuwa mkurugenzi mkuu wa majasusi wa M15 wa Uingereza zama zile alithibitisha kuwa madai haya ni uongo wala hayana ukweli.Ktk barua aliomuandikia gavana wa Kenya,Evelyn Baring tarehe 9:1:1953 alisema,
"Our sources have produced nothing to indicate that Kenyatta or his associates in the UK are directly involved in Mau Mau activities or that Kenyatta is essential to Mau Mau as a leader or that he is in a position to direct activities!"
(Source;Andrew pg 454)

Kufuatia amri na msukumo wa serikali yake ya Uk,Evelyn Baring aliendelea na kutangaza hali ya hatari 21:10:1952,na kuanzia kuwashika na kuwatesa wapinzani wa ukoloni na vibaraka.

Na kuwaeka ktk hali duni mbaya isio ya kibinadamu kufikia hadi kamishna wa polisi wa kikoloni Arthur Young,akamuandikia gavana wa Kenya zama zile Evelyn Baring barua mnamo 22:11:1954 akilalamika,
"The horror of some of the so-called Screening Camps now present a state of affairs so deplorable that they should be investigated without delay,so that the ever increasing allegations of inhumanity and disregard of the rights of the African citizen are dealt with and so that the government will have no reason to be ashamed of the acts which are done in its own name by its own servants."
(Source; Taking on The Boss:The Quiet Whistle Blowers on Events In Kenya Deserve Praise).

Kufuatia kusalitiwa na jamaa zao wenyewe,Mau Mau walitoa vitisho kwa Jomo Kenyatta, kutaka kumuua kwa kushirikiana na wakoloni kama alivyodhihirisha mwenyewe Kenyatta ktk hotuba yake April 1963,

"We are determined to have independence in PEACE,and we shall not allow HOOLIGANS to rule Kenya.
We must have no hatred towards one another .Mau Mau was a DISEASE which had been eradicated and must NEVER BE REMEMBERED again! (Source Clough 1998 p25).

Hivyo kupelekea kushikwa kwa hasimu na mpinzani wake mkuu, aliekuwa adui mkubwa wa wakoloni Dedan Kimathi,20:10:1956, hatimae kumuua kwa kumnyonga si yeye tu bali kila alojitolea muhanga kuwapinga na kupigana kidhati dhidi ya wakoloni na vibaraka(loyalists) wao ambao walituzwa kwa nyadhifa tofauti ktk serikali kuanzia pamoja na kugawiwa ardhi kubwa kama zawadi.

Jumamosi tarehe 12:12:2015,Kenya imesherehekea tena sherehe za jamhuri ikiwa ni za 52 tangu Kenya kutangazwa kuwa jamhuri 12:12:1964.Au kama raia wanavyohadaiwa na wakoloni na vibaraka wao.
Licha ya kuwa Kenya kuna kiongozi mmoja,bendera moja,wimbo wa taifa mmoja,court of arms moja,zote zikiashiria UMOJA.
Ukweli ni kuwa nchi imegawanyika tena vibaya Kwa misingi ya kimajimbo,maeneo,kikabila.Ili mtu awe rais Kenya,lazima awe na ushawishi mkubwa wa kabila lake bali kufaulu ni awe kiongozi wa kabila lake kamwe si ktk serikali wala upinzani.

Gonjwa hili lipo na tiba yake pekee ipo kwenye Uislam kama mfumo kamili wa maisha chini ya kivuli cha Khilafah.
Kwa sababu kivitendo Uislam ushalitokomeza kama bado Waislam wangali nalo ni matunda ya kutawaliwa na mfumo wa kikoloni ubepari democrazy.

DAWAH NI QAUL NA AMAL

Friday, December 11, 2015

MTAZAMO JUU YA UTEUZI WA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI KATIKA SERIKALI YA AWAMU YA 5 TANZANIA

HAIPUNGUZWI GHARAMA KWA KUPUNGUZA IDADI YA WATU BALI ZITAPUNGUZWA AU KUONDOLEWA GHARAMA KABISA KWA KUUONDOA UBEPARI.

Na Abdulrasheed Abdullah 
Mabepari huwa na kanuni ya kuwapa watu ufahamu wa kioo,yaani hulizungumzia jambo kwa sura ya kulia wakati kiuhalisia lipo kushoto.Kipimo kikubwa cha ubepari ni maslahi,kinachomsukuma mtu kufanya jambo ingawaje ukikitazama kwa jicho angavu utaona namna gani kilivyofeli.
Mfano,wakati watu wa Uropa wanaelekea kwenye mapinduzi ya viwanda,ilidhaniwa kwamba uzalishaji utaongezeka sambamba na gharama kupungua ikiwa kutapunguzwa gharama za uzalishaji zinazosababishwa hasa na utegemeaji wa nguvu za watu(labour) katika uzalishaji.Mbinu hii ya utumiaji wa nguvukazi(labour) sana kuliko mashine hujulikana kama labour intensive,
Hivyo wakapendekeza kutoitegemea sana mbinu hii ya nguvu kwenye uzalishaji na badala yake itumike mbinu mpya ya uzalishaji ambayo ni capital intensive ambapo mashine ndio huwa na nafasi kubwa kuliko binadamu.Matokeo hasi ya mbinu hii ni kuzidi kuongezeka tatizo la ajira ulimwenguni,watu milioni 10 wanaweza kukosa kazi kutokana na kutumiwa mashine moja tu kwenye uzalishaji.
Baada ya kushindwa kutatua tatizo la ajira ulimwenguni na kutaka kudhibiti mwamko wa watu ulimwenguni ili wasije wakachukua maamuzi ya kutaka kupora mali zinazomilikiwa na watu wachache(warasilimali),Program mpya ikaanzishwa ya kudhibiti vizazi ambapo mbinu nyingi zimetumika ndani yake kama Family planning,uzalishaji wa vimelea vya magonjwa,utengenezaji wa bidhaa zenye sumu,kuchochea vita na uhasama n.k
Yote haya wameyaleta ili kuweza kulinda maslahi yao yaani kupunguza ‪#‎Gharama‬.
Ajabu! mpaka leo wanaovikwa taji la usomi wanaendelea kufikiri na kudhania ndani ya mipaka ya duara waliolichora mabepari hawa wa Uropa,kuwa gharama hupungua kwa kupunguza idadi ya watu...
Kihakika MAGUFULI naye atashindwa kupunguza gharama kupitia njia hii ya kupunguza idadi ya mawaziri serikalini.
Ni jambo dogo tu yafaa kujiuliza,kwani gharama za elimu,afya,usafiri,umeme, unga,mchele,maharage,sukari,mafuta na bidhaa zote zinazozalishwa ndani ya nchi zimepanda kwa sababu ya kuwepo na mawaziri wengi?
Ukweli ni huu,kupunguza idadi ya mawaziri sio ndio njia ya kupunguza gharama za maisha kwa ummah unaoutawala.Hivi kuna nchi angalau moja imewahi kushuka deni la taifa mpaka kufikia 0%? na kama hakuna,je sababu wana mawaziri wengi?
Nahofia kadri muda utakapozidi kwenda bila ya kuuleta mfumo mbadala,linaweza likaletwa wazo la kutumia obot kuongoza nchi ili kupunguza gharama maana hakutokuwa na haja ya kumlipa mshahara....

Sunday, December 6, 2015

VITA VIKALI VYA KIELEKTRONIKI DHIDI YA HIZB UT-TAHRIR NA HATIMAYE KUFUNGWA KWA UKURASA WA FACEBOOK WA AMEER

Vita vikali vya kielektroniki dhidi ya Hizb ut Tahrir Na hatimaye kufungwa kwa Ukurasa wa Facebook wa Ameer wa Hizb ut Tahrir
 
Ijumaa, Des 04 2015 Kwa Vyombo Vya Habari
(Tafsir)
Tangu kutokea msururu wa visa vya mashambulizi ya kupangwa, vilivyojumuisha ushambuliaji wa risasi, kutekwa nyara mateka, katika Jiji la Paris nchini Ufaransa siku ya Ijumaa jioni, Novemba 13, 2015, njama za kiulimwengu zilitangazwa kupambana na tovuti za ISIS. Ajabu ilijumuisha na tovuti rasmi ya harakati ya Hizb ut Tahrir, chama cha kisiasa cha Kiislam ambacho hakitumii mabavu katika njia iliojifunga nayo, kufikia malengo yake, kwani haya yakiuka taratibu za Kisharia za kuleta mageuzi. Juu ya haya, tovuti yake ilijumuishwa miongoni mwa zile zenye kulengwa, licha kuwa Hizb ut Tahrir imekariri mara kadha katika matukio tofauti kuwa yapinga njia inayofuatwa na ISIS, na kuwa haina mafungamano ya ndewe wala sikio na ISIS. Lakini miungano na serikali zenye uadui dhidi ya Hizb ut Tahrir, hilo halikuwa pingamizi kwao kutofunga tovuti zake, dhihirisho la uadui na uhasama dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Jana Jumanne, 01/12/2015 saa 4:00 pm, usimamizi wa Facebook ulijitwika jukumu la kuondoa ukurasa wa mwanachuoni mkuu Sheikh Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, Ameer wa Hizb ut Tahrir, na kumfungia licha kuwa,ukurasa huo ulikuwa na nishati na wapendwa sana.Ulikuwa ukijadili matukio ya kila siku katika kila nyanja za kimaisha ima Kisiasa, Kifikra na Kithaqafa, Kifiqhi akijibu masuali kadha aliyotumiwa Ameer wa Hizb, huku Ummah ukimuamini, kielimu na kiufahamu wake wa kina alionao juu ya masuala tofauti.Kukiwa na watu wengi wenye kuipenda, kushirikiana na kutoa maoni yao tofauti tofauti huku idadi ya wanaoshiriki katika ukurasa wake ukizidi idadi ya watu 263,500. Jambo hili, likawakosesha lepe madhalimu na kuwapelekea kunoa ndimi zao za chuki na uhasama dhidi ya Uislamu na Waislamu hasa wabebaji wa ulinganizi wa Uislamu kwa usafi wake. Hivyo wakaanza kampeni kali dhidi ya ukurasa huo, kwa siku kumi kufuatana bila kuchoka.
Kando na kutuma barua kwa wasimamizi wa Facebook kuwasihi wasiufunge ukurasa huo, na kuwajulisha kuwa hatujapokea sababu yoyote ya kimsingi ya kuufunga ukurasa huo. Ajabu wasimamizi wa wa Facebook hawakujibu barua hiyo, badala yake wakasisitiza kuufunga ukurasa! Hili ladhihirisha kuwa ufungaji huu, ulifanywa kiuadui, bila kuwepo sababu yoyote muafaka, bali chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Kufungwa kwa ukurasa huo, wenye ucha Mungu na mafunzo ya hekima, ni moja wapo ya vita vya makufar vya msalaba dhidi ya Uislamu na Waislamu, kwa sababu yakuueleza Uislam kwa usafi wake, kama ulivyo teremshwa na Ar Rasul Muhammad (saw), na mtazamo safi na haki wa kisiasa ,unawafanya Waislamu kumtambua ndugu yao wa dhati mwenye kujitolea kuwahudumia licha ya kuviziwa na adui.
Daima dawama Kaffir wa kimagharibi, ana upangia njama ulinganizi safi wa Kiislamu, akidhani kwa kufanya hivyo atazuia nuru yake au, kuwaficha watu ukweli wake.Haya ni matokeo ya kupata hali ngumu na kukosa usingizi kwa ujumbe mzito wa harakati.Hivyo ikaamua kutumia silaha zake zote, kutumia uamuzi wa kikoloni uliopo mabongoni mwao,na kuwamrisha vibaraka wake wote na mamluki wake kuupiga vita Uislamu na Waislamu. Hata neno la kweli dogo kwao limekuwa tishio kubwa, likiwatia hofu na kuwa nyima usingizi.Hivyo wanawaamrisha majasusi wao wote,njama hizi mbovu, hatimaye kutumia uadui wao na chuki kufunga ukurasa huo mwema katika vita vya msalaba dhidi ya Uislamu na Waislamu.Lakini haya yote ni bure.Wala hawataweza kuizima Nuru ya Allah!
يُرِيدُونَ أَن يُطْفِؤُواْ نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّهُ إِلاَّ أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ * هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ
“Wataka kuizima Nuru Ya Allah kwa midomo yao,lakin Allah Akataa ila kuitimiza Nuru Yake hata kama makafir wachukia.Yeye Ndie Aliemtuma Mtume Wake na Uongofu na Dini Ya haki, ili idhihiri juu ya dini zote japo makafiri wachukia.”[At-Tawba: 32-33]

Toleo No: 1437 AH /010 Wednesday, 20th Safar 1437 AH 02/12/2015 CE

WAISLAM MTWARA NAO HAWAPO NYUMA KATIKA KULETA MABADILIKO


 Mwanaharakati wa hizb ut tahrir afrika mashariki Kaema Juma akiwa mjini mtwara alipokuwa kwenye ziara na akapata fursa ya kufanya semina ya misingi ya habari na uislamu kwa wanahabari wa kiislamu waliopo mji huo. Alikutana nao Masjid al Huda. Aliwasilisha mada na kupata nafasi ya kuulizwa maswali na wahudhuriaji wa semina hiyo